NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
MATAIFA mbalimbali yametakiwa kuweka mazingira mazuri ya kuwafanya wafanyakazi wahamiaji wanapotoka kwenye nchi zao wanakuwa na mazingira rafiki wakati wanapofanya kazi zao ili kuepuka mkanganyiko kwenye kazi.
Hayo yamebainishwa leo Desemba 18,2023 Jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA), Cde Hery Mkunda wakati wa kikao cha Mtandao wa wafanyakazi wahamiaji wa Afrika unafanyika chini ya Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi la Kimataifa.
Amesema katika kikao hicho ambacho washiriki 32 kutoka nchi za Afrika wameshiriki na kujadili namna ya kuweka mfumo rafiki ambao utaakisi wafanyakazi wanalindwa na kupata haki zao.
"Sisi kama wafanyakazi kupitia shirikisho la wafanyakazi Afrika tumeona ni muda muafaka kuungana wote kwa pamoja kushirikiana kuona jinsi gani tunaweka mazingira katika nchi zetu kuhakikisha tunawalinda hawa wafanyakazi wanapata haki zao, wanalindwa na kuhakikisha kwenye ajira zao wanapata haki za msingi ". Amesema
Aidha amesema kuwa wafanyakazi wahamiaji ili aweze kupata haki zao za msingi anapotoka nchini Tanzania kwenda nchi nyingine lazima awe salama na kulindwa.
0 Comments