Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania ( TPA) imezindua Rasmi Ofisi yake katika nchi ya Malawi ikiwa ni hatua ya Mamlaka hiyo kusogeza huduma za Bandari karibu na wateja wake wa nchini humo.
Waziri wa Uchukuzi wa Tanzania Mhe. Profesa Makame Mbarawa amesema, ofisi hiyo itapunguza usumbufu kwa wateja wa Bandari ya Dar es salaam kutoka nchini Malawi na watapata huduma zote wakiwa nchini mwao.
Kwa upande wake waziri wa Uchukuzi na ujenzi wa Malawi Mhe. Jacob Hara amesema, ofisi hiyo itakuwa na manufaa makubwa kwa wafanyabiashara wa Malawi na itarahisisha shughuli za usafirishaji wa mizigo kupitia bandari hiyo.
Mkurugenzi Mkuu wa TPA Bw. Plasduce Mbossa amesema uzinduzi wa ofisi hiyo unatimiza dhamira wa mamlaka hiyo kusogeza huduma zake kwa wateja wake.
0 Comments