Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Balozi Emmanuel John Nchimbi akiteta jambo na kumsikiliza kwa makini Bi. Fatma Gullam Hussein Jamal (Mama Fatma Karume), ambaye ni Mama Mzazi wa Rais Mstaafu wa Zanzibar, Dkt. Amani Abeid Karume (kulia), pia Mjane wa Rais wa Kwanza wa Zanzibar, Hayati Abeid Amani Karume, walipokutana msibani kwa Hayati Edward Ngoyai Lowassa, Ngurash, Monduli, Jumamosi, Februari 17, 2024. Dkt. Nchimbi pia alitumia nafasi hiyo kumpongeza Mama Fatma Karume kwa kutimiza miaka 93 ya kuzaliwa hivi karibuni na kumtakia heri, fanaka na maisha marefu zaidi.
0 Comments