NA EMMANUEL MBATILO
SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS) kanda ya ziwa limetoa elimu kwa umma kuhusiana na usalama wa chakula kwa lengo la kuhakikisha walaji wanatumia chakula salama kufutia kuwepo kwa vihatarishi vya mlipuko wa magonjwa ya kipindupindu jijini Mwanza.
Akizungumza leo Februari 8,2024 Afisa Udhibiti Mwandamizi wa TBS Bi.Nuru Mwasulama amesema TBS imekua inatoa elimu kuhusiana na umuhimu wa chakula salama.
Aidha amesema kuwa wamekuwa wakifundisha kanuni za kufuata katika kufikia chakula salama ikiwemo kunawa mikono kwa maji tiririka na sabuni kabla ya kuandaa na kula chakula na pia uhifadhi bora wa chakula.
Amesema chakula kinatakiwa kisichanganywe wala kuwekwa kwenye kemikali kwani chakula kinatakiwa kuwekwa kwenye jokofu kwasababu chakula ambacho cha kuharibika haraka usipoweka kwenye joto linalotakiwa, wadudu wanaota na kuchafua chakula.
"Mara nyingine huchafuzi huu hauonekani kwa macho, vimelea kama bakteria hauwezi kuona kama chakula kimechafuliwa mpaka upime, hivyo kuna umuhimu wa kunawa mikono kwa maji tiririka na sabuni". Amesema
Pamoja na hayo amesema matumizi ya maji salama kwa ajili ya kunywa husaidia kuepukana na magonjwa ya mlipuko kama kipindupindu.
0 Comments