Ticker

6/recent/ticker-posts

WATUMISHI NGAZI YA MSINGI SERIKALI ZA MTAA WANOLEWA KUUNDA BAJETI ZENYE MLENGO WA JINSIA

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

WATUMISHI ngazi ya msingi Serikali za Mitaa,wametakiwa kuwasaidia wananchi hasa wanawake kushiriki katika masuala ya Uongozi na kuandaa bajeti ambazo zinazingatia usawa wa kijinsia.

Wito huo umetolewa leo Februari 19,2024 Jijini Dar es Salaam na Naibu Mkuu wa Chuo Cha Serikali za Mitaa Hombolo, Dkt. Lazaro Kisumbe akimwakilisha Mkuu wa chuo Cha Serikali za Mitaa Kwenye Uzinduzi wa Mafunzo ya Ukondoishaji wa masuala ya kijnsia pamoja na uandaaji wa bajeti zenye mlengo wa kijinsia.

Aidha amesema kuwa mafunzo hayo yamelenga kuwapatia Elimu na ujuzi ambao utawasaidia wanawake katika ngazi ya jamii kushiriki katika masuala ya Uongozi na uchumi.

"Mafunzo haya yanalenga (ukondoishaji) yaani ujumuishaji wa masuala ya kijinsia jinsia kwa kuzingatia usawa kwenye sera na mipango,lakini suala la pili kwenye haya mafunzo yanalenga bajeti zinazo zingatia mahitaji ya usawa wa kijinsia "Dkt.Kisumbe amesema.

Amesema mafunzo hayo yamekuja kutokana na matokeo ya utafiti ulifanywa mwaka 2022 ambapo yamethibitisha wanawake asilimia 3 pekee katika ngazi za mitaa ndio wanajishughulisha na masuala ya Uongozi na kiuchumi.

Pamoja na hayo ameeleza kuwa wanatatarajia kuona mabadiriko makubwa kutokana na mafunzo hayo kwa kuondoaa ombwe kubwa la wanawake ambao hawajihusishi na masuala ya Uongozi na uchumi kwa madhumuni ya kuondoa umaskini.

"Tunaimani kwamba hamkuja kwa bahati mbaya,wamewachagua watu sahihi,mkitoka hapa mtaonesha kwamba mlipata fursa stahiki mtaenda kuacha alama kwa kuhakikisha mnaleta mabadiriko ya ukondoishaji kwa jamii lakini pia kwa kuandaa bajeti zinazozingatia mahitaji ya kijinsia"Dkt.Kisumbe ameeleza.

Kwa Upande wake, Mkuu wa Idara Maendeleo ya Jamii na Mratibu wa Mradi wa Women Leadership and Economic Rights (WLER), Dkt. Benedict Sulley amesema usawa wa kijinsia katika ngazi ya msingi umeonekana kuwa chini ya asilimia 3 jambo ambalo ni hatari kwa maendeleo ya nchi kwani wanawake kitakwimu ni wengi kuliko wanaume.

Naye Mkurugenzi wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP)Bi.Lilian Liundi amesema mafunzo hayo yatasaidia kujenga uelewa mpana wa dhana ya kijinsia,kubainisha fursa zilizopo katika ngazi za mtaa na kutambua mifumo ambayo inazuia ushiriki wa Wanawake katika Uongozi na Shughuli za uzalishaji mali kwa lengo la kupata mbinu za kuongeza ushiriki wa Wanawake katika masuala hayo.

Aidha Bi. Liundi amebainisha kuwa haki za binadamu na za wanawake bado zinajadiliwa kwa sababu wanawake hawajawa kwenye nafasi na fursa sawa kama wanaume katika jamii.

"Bado wananyanyaswa na kukandamizwa na kuonewa na mifumo ya maisha iliyopo haki za binadamu na za wanawake ni pamoja na haki za kiutamaduni, kiuchumi, kijamii, kisiasa na haki za kiraia. Masuala yanayoashiria wanawake kuwa mstari wa mbele katika kuwepo mgawanyo mzuri wa kazi kijinsia na rasilimali hali ambayo kwa Sasa haipo"Bi.Liundi amesema

Mafunzo hayo yatafanyika kwa siku nne kuanzia Februari 19-22,2024 katika Viunga vya ofisi ya Mtandao wa Jinsia yakiendeshwa na wawezeshaji kutoka TGNP kwa Kushirikiana na Chuo Cha Serikali za Mitaa-Hombolo na UN Women.
Naibu Mkuu wa Chuo Cha Serikali za Mitaa Hombolo, Dkt. Lazaro Kisumbe akizungumza katika mafunzo ya Ukondoishaji wa masuala ya kijnsia pamoja na uandaaji wa bajeti zenye mlengo wa kijinsia yaliyofanyika leo Februari 19,2024 katika ukumbi wa TGNP Mtandao Jijini Dar es Salaam.
Naibu Mkuu wa Chuo Cha Serikali za Mitaa Hombolo, Dkt. Lazaro Kisumbe akifungua mafunzo ya Ukondoishaji wa masuala ya kijnsia pamoja na uandaaji wa bajeti zenye mlengo wa kijinsia yaliyofanyika leo Februari 19,2024 katika ukumbi wa TGNP Mtandao Jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Idara Maendeleo ya Jamii na Mratibu wa Mradi wa Women Leadership and Economic Rights (WLER), Dkt. Benedict Sulley akizungumza katika mafunzo ya Ukondoishaji wa masuala ya kijnsia pamoja na uandaaji wa bajeti zenye mlengo wa kijinsia yaliyofanyika leo Februari 19,2024 katika ukumbi wa TGNP Mtandao Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP)Bi.Lilian Liundi akizungumza katika mafunzo ya Ukondoishaji wa masuala ya kijnsia pamoja na uandaaji wa bajeti zenye mlengo wa kijinsia yaliyofanyika leo Februari 19,2024 katika ukumbi wa TGNP Mtandao Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) Bi.Lilian Liundi akisisitiza jambo wakati wa mafunzo ya Ukondoishaji wa masuala ya kijnsia pamoja na uandaaji wa bajeti zenye mlengo wa kijinsia yaliyofanyika leo Februari 19,2024 katika ukumbi wa TGNP Mtandao Jijini Dar es Salaam.
Watumishi ngazi ya msingi Serikali za Mitaa wakiwa kwenye mafunzo ya Ukondoishaji wa masuala ya kijnsia pamoja na uandaaji wa bajeti zenye mlengo wa kijinsia yaliyofanyika leo Februari 19,2024 katika ukumbi wa TGNP Mtandao Jijini Dar es Salaam.

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

Post a Comment

0 Comments