Na Munir Shemweta, KATAVI
Mbunge wa Jimbo la Kavuu na Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe, Geophrey Pinda amewataka wanawake katika halmashauri ya Mpimbwe katika wilaya ya Mlele mkoa wa Katavi kuhakikisha wanaimarisha vikundi vyao vya ujasiriamali ili kwa lengo la kujiletea maendeleo.
Mhe, Pinda ametoa kauli hiyo katika kata ya Mwamapuli halmashauri ya Mpimbwe mkoa wa Katavi wakati wa sherehe ya wanawake kuelelea siku ya wanawake duniani inayoadhimishwa kila mwaka mwezi Machi 3.
Halmashauri ya Mpimbwe imeweka utaratibu wa kupeleka maafisa wake katika kila kata inayofanya sherehe za siku ya wanawake kwa lengo la kupokea kero za wanawake na baadaye kuzitafutia ufumbuzi.
Mbunge huyo wa jimbo la Kavuu amewata wanawake hao kuweka utaratibu ikiwemo kuwa na uongozi imara wa vikundi utakaowezesha vikundi hivyo kutunza fedha na kufanya biashara itakavyovipa faida.
Aidha, amewataka maafisa kutoka halmashauri ya Mpimbwe hasa wale wanaohusika na mikopo kuhakikisha wanatoa elimu ya kutosha kwa vikundi vya wanawake ili vijielewe katika zile shughuli zinazokwenda kufanya.
‘’Hivi vikundi vya akina mama vikijiimarisha na kuwa sambamba na kuwa na uongozi imara vinaweza kufanya mambo makubwa kupitia biashara wanayoweza kuifanya kupitia vikundi’’ alisema Mhe, Pinda
Mhe, Pinda ametolea mfano katika halmashauri ya Mpimbwe ambayo ni maarifu kwa uzalishaji Mpunga na Mahindi kuwa, vikundi katika halmashauri hiyo vinaweza kufanya biashara kwa kufuata mpunga mashambani na baadaye kuuza kwa wafanyabiashara jambo alilolieleza kuwa linaweza kuwapa faida kubwa.
Mbunge wa Jimbo la Kavuu na Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe, Geophrey Pinda akizungumza na wanawake wa Kata ya Mwamapuli halmashauri ya Mpimbwe wilaya ya Mlele mkoa wa Katavi wakati wa sherehe ya siku ya wanawake katika kata hiyo.
Sehemu ya wanawake wa Kata ya Mwamapuli halmashauri ya Mpimbwe wilaya ya Mlele mkoa wa Katavi wakimsikiliza Mbunge wa Jimbo la Kavuu na Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe, Geophrey Pinda (hayupo pichani) wakati wa sherehe ya siku ya wanawake katika kata hiyo.
0 Comments