Na Mwandishi Wetu, Tanga
MADEREVA bodaboda wapatao 300 waliopo katika Jiji la Tanga wamepatiwa mafunzo ya usalama barabara yenye lengo la kusaidia kumaliza changamoto ya ajali ya barabara .
Mafunzo hayo hayo yanayofadhiliwa na ubalozi wa Uswizi kupitia shirika la Amend yamelenga kutoa elimu ya usalama barabara kwa kushiriki na kikosi Cha usalama barabara mkoani humo.
Akizingumza wakati wa utolewaji mafunzo kwa vitendo kwa madereva wa bodaboda wa Jiji hilo Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Tanga William Mwamasika amesema kupitia mafunzo hayo wataelimisha kanuni na sheria za usalama barabara kwa lengo la kinawashukuru bodaboda kujilinda na ajali za barabarani.
Amesema kwa kushirikiana na AMEND wamejipanga kutoa mafunzo hayo katika Wilaya zote za Mkoa wa Tanga."Tunajua
hawa bodaboda wakipatiwa mafunzo ya usalama barabara ajali zitapungua kwa kiwango kikubwa,"amesema Mwamasika.
Pia amesema kupitia mafunzo hayo itasaidia madereva hao kuzifahamu sheria za usalama barabarani na kuzitii alama hizo,hivyo kupunguza vitendo vya uvunjifu wa sheria ikiwemo kupakiza zaidi ya abiria mmoja.
"Kundi hili ni muhimu sana katika kupatiwa elimu hii kwani wamekuwa ni sehemu ya wahanga wa ajali sambamba na uvunjifu wa kanuni za usalama wawapo barabarani,"amesema Kamanda huyo.
Kwa upande wao baadhi ya madereva wa bodaboda waliopatiwa mafunzo wamesema mafunzo hayo yamewasaidia kuongeza uwelewa kuhusu matumizi sahihi ya Sheria za usalama barabarani sambamba na kuzingatia alama na hivyo kutii sheria bila shuruti.
Dereva bodaboda Abdallah Juma amesema mafunzo hayo yamewasaidia kuwaongezea umakini wawapo barabarani hivyo wanatoa shukrani kwa AMEND na Ubalozi wa Uswisi kwa kufanikisha mafunzo hayo.
Wakati huo huo dereva bodaboda Ali Ramadhani ameeleza ajali nyingi zinazotokea barabarani zinatokana uzembe wa madereva wa pikipiki."Kwa mafunzo tuliyopata yatasaidia kukabiliana na makosa mbalimbali wakiwa barabarani."
0 Comments