Ticker

6/recent/ticker-posts

PLAN INTERNATIONAL YATOA MSAADA WA VIFAA SAIDIZI TAB VYENYE THAMANI YA ZAIDI YA SH. MILIONI 9

EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

MSTAHIKI Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni Mhe. Songoro Mnyonge amelipongeza Shirika la Plan International kwa kutoa msaada wa vifaa saidizi kwa Jumuiya ya Wasioona Tanzania ( TAB) vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 9.

Akizungumza katika hafla ya makabidhiano hayo leo Machi 21,2024 katika Ofisi za (TAB) Jijini Dar es Salaam, Mhe. Mnyonge amesema wasioona wanapitia wakati mgumu pindi wanapokosa vifaa saidizi ambavyo vingeweza kuwasaidia kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingini.

"Nimesikia kuna wengine wametokea Buza, Kigamboni, Goba na maeneo mengine ya mbali na kufika hapa ofisini kwao, wamekuwa wakipatiwa msaada na wananchi wa maeneo ya Kinondoni kufika kwenye neoe hili la ofisi, hivyo basi kuna umuhimu wakamata vifaa saidizi". Amesema Mstahiki Meya Mnyonge.

Kwa upande wake Mkuu wa idara ya mawasiliano na uchechemuzi Shirika la Plan International  Bi. Cecilia Bosco amesema vifaa hivyo vitawasaidia kutoka kwenda katika Shughuli zao za kila siku za kujipatia kipato.

Aidha amesema wameipatia taasisi ya watu wasioona vifaa ambavyo ni fimbo nyeupe 100,Karatasi za kijivu pisi 100 pamoja na A4 fremu pisi 50 ambazo hutumika wanapokuwa wanaandika ambazo itawasaidia katika shughuli zao.

Amesema wataendelea kuimarisha nakuongeza nguvu kuwasaidia watu wasioona pamoja na makundi mbalimbali yenye mahitaji maalumu nchini kwa lengo la kupunguza changamoto wanazozipitia.

Naye Mtunza hazina wa Jumuiya ya watu wasioona Tanzania Bw.Seif Hamis amesema vifaa hivyo ni muhimu sana ambapo itawasaidia kuzifikia fursa mbalimbali.

Aidha ameishukuru serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Dkt. Samia Suluhu Hassan ambapo imefungulia  milango ya fursa mbalimbali kama watu wasioona.

Mkuu wa idara ya mawasiliano na uchechemuzi Shirika la Plan International  Bi. Cecilia Bosco (kulia) akimkabidhi Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni Mhe. Songoro Mnyonge baadhi ya vifaa saidizi ambavyo vimegawiwa kwa Jumuiya ya Wasioona Tanzania ( TAB). Hafla hiyo imefanyika leo Machi 21,2024.
Mkuu wa idara ya mawasiliano na uchechemuzi Shirika la Plan International  Bi. Cecilia Bosco (kulia) akimkabidhi Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni Mhe. Songoro Mnyonge baadhi ya vifaa saidizi ambavyo vimegawiwa kwa Jumuiya ya Wasioona Tanzania ( TAB). Hafla hiyo imefanyika leo Machi 21,2024.
Mkuu wa idara ya mawasiliano na uchechemuzi Shirika la Plan International Bi. Cecilia Bosco (kulia) akimkabidhi Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni Mhe. Songoro Mnyonge baadhi ya vifaa saidizi ambavyo vimegawiwa kwa Jumuiya ya Wasioona Tanzania ( TAB). Hafla hiyo imefanyika leo Machi 21,2024 Jijini Dar es Salaam.
Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni Mhe. Songoro Mnyonge akikabidhi baadhi ya vifaa saidizi kwa Mtunza hazina wa Jumuiya ya watu wasioona Tanzania Bw.Seif Hamis ambavyo vimetolewa na Shirika la Plan International leo Machi 21,2024 Jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa idara ya mawasiliano na uchechemuzi Shirika la Plan International  Bi. Cecilia Bosco akizungumza mara baada ya kukabidhi vifaa saidizi kwa Jumuiya ya Wasioona Tanzania ( TAB) leo Machi 21,2024 Jijini Dar es Salaam.
Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni Mhe. Songoro Mnyonge akizungumza katika hafla ya magabidhiano ya msaada wa vifaa saidizi kwa Jumuiya ya watu wasioona Tanzania, ambavyo vimetolewa na Shirika la Plan International leo Machi 21,2024 Jijini Dar es Salaam.
Mtunza hazina wa Jumuiya ya watu wasioona Tanzania Bw.Seif Hamis akizungumza mara baada ya kupokea msaada wa vifaa saidizi vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 9 kutoka Shirika la Plan International leo Machi 21,2024 Jijini Dar es Salaam.
Wanachama wa Jumuiya ya Wasioona Tanzania ( TAB) wakiwa kwenye picha ya pamoja na Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni Mhe. Songoro Mnyonge pamoja na wawakilishi kutoka Shirika la Plan International mara baada ya Shirika hilo kukabidhi msaada wa vifaa saidizi kwa TAB leo Machi 21,2024 Jijini Dar es Salaam.

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

Post a Comment

0 Comments