NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
TAASISI ya HakiElimu imependekeza kwa Serikali kupitia Wizara ya Elimu kutenga Bajeti mahususi kwaajili ya kuhuisha mpango wa tatu wa Maendeleo ya Sekta ya elimu au kuandaa mpango wa nne wa Maendeleo ya Sekta ya elimu katika mwaka wa fedha mpya kwenye sera na Mtaala husika.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Aprili 23, 2024 Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa HakiElimu, John Kalage alisema serikali inapoelekea katika upangaji wa Bajeti ya Sekta ya elimu kwa mwaka wa fedha 2024/25 inapaswa kuzingatia mchakato wa utengenezaji wa Dira ya maendeleo ya Taifa 2025 lakini pia kuanza kwa utekelezaji wa mitaala na sera mpya ya elimu 2023.
Aidha amesema Serikali kupitia ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za mitaa (TAMISEMI) imeongeza Tahasusi mpya 49 za kidato Cha Tano kutoka 16 zilizokuwepo awali hadi kufikia Tahasusi 65.
"Kama serikali inakusudia kuanza utoaji wa Tahasusi hizo zote ni muhimu kupanga na kutenga Bajeti maalum katika mwaka wa fedha 2024/25 kwaajili ya mambo mbalimbali ikiwemo kutoa mafunzo kazini kwa walimu waliopo, kuajiri walimu wapya wenye ujuzi na umahiri katika Tahasusi husika lakini pia kuwa na mpango maalumu wa Kuhamasisha udahili wa wanafunzi wa ualimu vyuoni ili kuendelea kutengeneza walimu wenye ujuzi kulingana na mabadiliko hayo". Amesema
Pamoja na hayo, HakiElimu imependekeza pia Bajeti kwaajili ya uchapaji na usambazaji wa vitabu vya Kiada shuleni, ambapo wameiomba serikali katika Bajeti ya Sekta ya elimu mwaka wa fedha 2024/25 watenge Bajeti maalumu kwaajili ya uchapaji na usambazaji wa vitabu hivyo mashuleni hasa kwa kuzingatia kuwa vitabu hivyo ni vipya hivyo shule hazina akiba ya vitabu mbadala.
Pia wameiomba serikali kuweka mpango maalumu wa usambazaji wa vitabu hivyo mashuleni ukiainisha muda mahususi wa ukamilishaji wa zoezi hilo
Mbali na hayo, Hakielimu wamependekeza ujumuishi wa teknolojia katika utekelezaji wa mtaala mpya wa Elimu, ambapo imeishauri serikali kupitia Wizara za Sekta ya elimu kutenga Bajeti kwaajili ya uboreshaji wa miundombinu ya shule ya msingi na sekondari ili kuziandaa na utoaji wa Elimu kwa Mtaala mpya na matumizi ya teknolojia.
Vilevile HakiElimu imependekeza Serikali itenge Bajeti kwaajili ya ununuzi wa vifaa vya kujifunzia na kufundishia vya teknolojia lakini pia kuanzisha vipindi vya ujuzi wa matumizi ya mtandao ili kuwawezesha wanafunzi kuwa na umahiri wa kutumia mtandao kwa usahihi, uwezo wa kutatua matatizo na uwezo wa kujifunzia.
Mkurugenzi Mtendaji wa HakiElimu, John Kalage (katikati) akizungumza na waandishi wa habari leo Aprili 23, 2024 wakati wakitoa mapendekezo juu ya upangaji na utendaji bajeti ya sekta ya Elimu ya Mwaka wa Fedha 2024/25.
Mkurugenzi Mtendaji wa HakiElimu, John Kalage (katikati) akizungumza na waandishi wa habari leo Aprili 23, 2024 wakati wakitoa mapendekezo juu ya upangaji na utendaji bajeti ya sekta ya Elimu ya Mwaka wa Fedha 2024/25.
Mkurugenzi Mtendaji wa HakiElimu, John Kalage akizungumza na waandishi wa habari leo Aprili 23, 2024 wakati wakitoa mapendekezo juu ya upangaji na utendaji bajeti ya sekta ya Elimu ya Mwaka wa Fedha 2024/25.
Mkurugenzi Mtendaji wa HakiElimu, John Kalage akisisitiza jambo wakati akizungumza na waandishi wa habari leo Aprili 23, 2024 wakati wakitoa mapendekezo juu ya upangaji na utendaji bajeti ya sekta ya Elimu ya Mwaka wa Fedha 2024/25.
Mkuu wa Miradi HakiElimu, Godfrey Boniventura akizungumza na waandishi wa habari leo Aprili 23, 2024 wakati wakitoa mapendekezo juu ya upangaji na utendaji bajeti ya sekta ya Elimu ya Mwaka wa Fedha 2024/25.
Meneja Idara ya Utafiti, Uvumbuzi na Uchambuzi wa Sera- Hakielimu, Bw. Makumba Mwemezi akizungumza na waandishi wa habari leo Aprili 23, 2024 wakati wakitoa mapendekezo juu ya upangaji na utendaji bajeti ya sekta ya Elimu ya Mwaka wa Fedha 2024/25.
(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)
0 Comments