NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
Taasisi ya ShuleSoft imezindua mradi wake wa toleo jipya,unaojihusisha na usimamizi wa shule, ambapo imelenga kusaidia masuala ya utawala, taaluma,mambo ya kifedha, mawasiliano,na kurahisisha ujifunzaji kwa mfumo wa kidigitali wa ShuleSoft.
Akizungumza na waandishi wa habari,leo Jijini Dar es Salaam April 09,2024 wakati wa uzinduzi wa toleo jipya la mradi huo, Mkurugenzi wa ShuleSoft Bw.Ephraim Swilla amesema wamefanya maboresho ya mradi huo kuongezea baadhi ya vipengele ambavyo havikuwepo awali kutokana na mapendekezo ya wateja wao.
Aidha ameeleza kuwa toleo hilo jipya limeunganisha wadau mbalimbali zikiwemo benki na mitandao ya simu ambapo itarahisisha kutoa suluhu ya changamoto za malipo shuleni na kuokoa muda kwa utawala, wazazi pamoja na wanafunzi
Amesema mradi wa toleo hilo jipya la shulesoft unakwenda kusaidia,masuala ya usimamizi wa shule katika nyanja mbalimbali ambazo ni mahudhurio, Maktaba ,bweni,taaluma,mawasiliano ya moja kwa moja na wazazi pamoja na uwajibikaji wa wafanyakazi.
"Shule sasa wanaweza kusimamia mambo ya mahudhurio,Maktaba,bweni lakini tuna kipengele cha kutuma mawasiliano kwa wazazi ambapo tumeuunganisha na Whatsapp, Telegram ikiwepo aplikesheni mpya ya simu inayoitwa (shule soft parent Experience) ambapo mzazi atajua kila kitu kinachoendelea shuleni"Bw. Swilla amesema
Pamoja na hayo ametoa onyo kwa watu wanaoiba kazi za wabunifu nakufanya udanganyifu kwa shule na kuharibu ubunifu wao uliofanyika kwa kutumia jina la taasisi hiyo vibaya na kutengeneza taswira mbaya kwa jamii kwa kujiingizia mapato yasiyo halali.
Pamoja na hayo ametoa wito kwa wadau wote wa elimu kuungana kufikisha kileleni taaluma ya nchi hii katika viwango vya kimataifa na amewaalika wadau kutoka shule za Umma na za binafsi ambazo hazijajiunga na mfumo huo wa shulesoft kufikia ofisi zao zinazopatikana Dar es Salaam, Arusha na Mbeya.
0 Comments