Ticker

6/recent/ticker-posts

ELIMU YA BIMA YATOLEWA KWA TAKUKURU KANDA YA ZIWA

Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania kupitia Kanda ya Ziwa imetoa elimu ya bima kwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU Mkoani Mwanza ambapo jumla ya watumishi wapatao 26 wameshiriki mafunzo hayo.

Mada mbalimbali ziliwasilishwa ikiwemo Majukumu ya TIRA, Dhana ya Bima, Bima za Magari, Taratibu za madai, Umuhimu wa kuwa wakala wa bima na bima za Nyumba. Aidha, mafunzo hayo yamefunguliwa na Mkuu wa Takukuru Mkoani hapa Kamanda James Ruge na kuhitimishwa na Naibu Kamanda Idrisa Kisaka.

Mafunzo yaliyotolewa ni muhimu katika kutekeleza Mpango Mkakati wa Utoaji Elimu Kitaifa NIES ambapo TAKUKURU ni miongoni kwa Taasisi mojawapo ya kimkakati TIRA KWA SOKO SALAMA LA BIMA

Post a Comment

0 Comments