Ticker

6/recent/ticker-posts

TBS YASHIRIKI MKUTANO WA 26 WA WAKUU WA MASHIRIKA YA VIWANGO AFRIKA MASHARIKI

MKURUGENZI Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) amesema kupitia Mkutano wa 26 wa wakuu wa mashirika ya Viwango ya Afrika Mashariki wanatarajia kupitisha viwango zaidi ya 102 vya bidhaa za Jumuiya ya Afrika Mashariki,na viwango 99 vya kimataifa vilivyotokana na Kamati za kiufundi.

Ameyasema hayo leo Mei 8, 2024 wakati wa Mkutano huo uliofanyika Jijini Arusha na kuhudhuriwa na wakuu wa mashirika ya viwango na udhibiti ubora kutoka nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

"Viwango hivi vimeandaliwa katika maeneo ya chakula,mbao,mazao ya pamba(nguo),Petrol na mazao yake,viatu,ngozi na mazao yake,mazo ya chuma,vifaa tiba, vipodozi na huduma". Amesema Dkt. Nyenya

Aidha amesema kuwa viwango hivyo ni muhimu katika kufanikisha biashara katika Jumuiya ya Afrika Mashariki na Afrika Kwa ujumla ili kuondoa vikwazo vya kiufundi jambo ambalo litachochea ukuaji wa uchumi wa nchi hizo.

Pamoja na hayo amesema mkutano huo utapokea taarifa za Kamati za kitaalamu katika maeneo ya viwango, udhibiti ubora, metrolojia, upimaji, Kamati ya codex na kamati ya kupunguza vikwazo vya kiufundi katika kibiashara pamoja na taarifa ya kikosi kazi cha kupitia mpango mkakati, uandaaji wa kanuni na utekelezaji wake.

Dkt.Ngenya amesema kuwa wakuu wa mashirika ya viwango na udhibiti ubora Afrika Mashariki watazipitia taarifa hizo na kuzifanyia kazi, ambapo mapendekezo mengine yatapelekwa kwenye vikao vya baraza la mawaziri la biashara, uwekezaji, fedha na viwanda kwa maamuzi zaidi kwa ajili ya kusaidia ufanyaji wa biashara katika jumuiya ambayo kwa sasa ina nchi wanachama nane baada ya Somalia kujiunga na kukidhi matakwa ya kuwa mwanachama.

Post a Comment

0 Comments