Ticker

6/recent/ticker-posts

NAIBU WAZIRI MNYETI ATEMBELEA BANDA LA TVLA KWENYE MAONESHO MNADA WA MIFUGO 2024

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Alexandar Mnyeti (wa pili kutoka kulia) akipata elimu kuhusiana na matumizi sahihi ya Chanjo za Mifugo zinazozalishwa na TVLA kutoka kwa Dkt. Fred Makoga (kushoto) Daktari Utafiti Mifugo wa Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania (TVLA) Juni 14, 2024 alipotembelea banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwenye maonesho ya Mnada wa Mifugo 2024 yanayofanyika kuanzia Juni 14 hadi 16, 2024 kwenye shamba la Mkonge la Highland Estate lililopo Chalinze Ubena Zomozi Mkoa wa Pwani.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Alexandar Mnyeti akipata elimu kuhusiana na uchambuzi na uhakiki wa ubora wa vyakula vya Mifugo kutoka kwa Afisa Utafiti Mifugo wa Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania (TVLA) Bw. Msafiri Kalloka (kushoto mwenye kofia) Juni 14, 2024 alipotembelea banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwenya maonesho ya Mnada wa Mifugo 2024 yanayofanyika kuanzia Juni 14 hadi 16, 2024 kwenye shamba la Mkonge la Highland Estate lililopo Chalinze Ubena Zomozi Mkoa wa Pwani.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Alexandar Mnyeti (alievaa shati jeupe) akijadiliana jambo na viongozi wakuu wa Wizara namna ya kuboresha upatikanaji wa huduma zinazotolewa na Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania (TVLA) kwa wafugaji Juni 14, 2024 walipotembelea banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwenya maonesho ya Mnada wa Mifugo 2024 yanayofanyika kuanzia Juni 14 hadi 16, 2024 kwenye shamba la Mkonge la Highland Estate lililopo Chalinze Ubena Zomozi Mkoa wa Pwani. Kushoto kwake ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo) Prof. Daniel Mushi.
Afisa Mtafiti Mifugo wa Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania (TVLA) Bw. Msafiri Kalloka akitoa elimu kuhusiana na matumizi sahihi ya Chanjo za Mifugo zinazozalishwa na TVLA kwa wadau wa Mifugo waliotembelea banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi Juni 14, 2024 kwenya maonesho ya Mnada wa Mifugo 2024 yanayofanyika kuanzia Juni 14 hadi 16, 2024 kwenye shamba la Mkonge la Highland Estate lililopo Chalinze Ubena Zomozi Mkoa wa Pwani.
Daktari Mtafiti wa Mifugo wa Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania (TVLA) Dkt. Fred Makoga (kushoto) akitoa elimu kuhusiana na uchunguzi na utambuzi wa Magonjwa ya wanyama kwa wadau wa Mifugo waliotembelea banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi Juni 14, 2024 kwenya maonesho ya Mnada wa Mifugo 2024 yanayofanyika kuanzia Juni 14 hadi 16, 2024 kwenye shamba la Mkonge la Highland Estate lililopo Chalinze Ubena Zomozi Mkoa wa Pwani.

Post a Comment

0 Comments