NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
SERIKALI kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imesema itaendelea kusimamia ufanyaji wa mtihani wa mwisho kwa walimu wa kuwapima ubora wao na kuwapa leseni kama ilivyo taaluma zingine kwa lengo la kuwaongezea thamani na kupata haki sawa ya ajira.
Ameyasema hayo Juni 25, 2024 Jijini Dar es Salaam, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda wakati wa hafla ya utoaji tuzo kwa walimu walioshinda shindano la pili la Stadi za kufundisha somo la Kiingereza kwa shule za msingi nchini ambapo tuzo hizo ziliandaliwa na Taasisi ya Elimu Tanzania (TET).
Amesema walimu ni yenye thamani kubwa nchini hivyo wataendelea kuiweke mazingira mazuri wakati wote, kuendelea kuwapa heshima kwa kazi kubwa wanayoifanya ya kujenga jamii yenye ya wasomi.
Aidha amesema Wizara itajitahidi kufanya afua mbalimbali za kuboresha mazingira ya walimu nchini, kufanikisha lengo huku akisema wanakazi kubwa katika kuboresha mazingira kuonyesha kuwa wanawathamini walimu.
"Tutaendelea kutenga fedha za kuwaendeleza walimu kusoma kufikia katika malengo yao ya kujiendeleza zaidi, na pia tutatumia kila hatua kuhakikisha tunaboresha mazingira ikiwemo kuwapa fursa mbalimbali ikiwemo semina pamoja na mikopo". Amesema Prof. Mkenda
Pamoja na hayo amesema "Sheria unasoma unapata shahada na kupatiwa mtihani, udaktari, uhasibu wanapimwa Kwa mtihani kutokana umuhimu wao, hivyo hata walimu kupitia sera imeelekeza namna ambavyo watakao hitaji kujiajiri watapewa mtihani".
Amesema kiswahili kitaendelea kuwa lugha kidedea nchini, bila kusahau lugha ya Kiingereza nchini kwani ndio lugha ya kimataifa .
Hata hivyo amesema wakati wakiendelea kubidhaisha kiswahili ni lazima lugha ya Kiingereza itumike hivyo ndiyo maana wanaendelea kuliwekea mazingira mazuri na vilevile ili tuweze kukuza lugha kiswahili lazima tuelewe vizuri lugha ya Kiingereza, kufikisha adhima.
"Hata kama tunapenda sana kiswahili hatuwezi kumudu kukisambaza vyema duniani hatuwezi kufanikisha kukifikisha katika mataifa mbalimbali ikifuatiwa na lugha zingine za kifaransa na zinginezo kufanikisha lengo". Amesema
Prof. Mkenda ameipongeza TET, kwa kazi kubwa waliyoifanya ya utoaji wa tuzo kwa walimu walioshinda shindano la pili la stadi za kufundisha somo la kiingereza kwa shule za msingi kwani inaenda kuleta motisha kwa walimu kufanya vizuri zaidi katika ufundishaji.
Vilevile amewapongeza walimu kwa ubunifu wao mkubwa katika kubuni mbinu za ufundishaji kuhakikisha wanafunzi wanapata uelewa mkubwa katika masomo husika na kuweza kufanya vizuri kwenye masomo yao.
Kwa upande wake Mwakilishi wa benki ya Dunia, Muna Meka ameipongeza TET kupitia Wizara ya Elimu, kwa ubunifu mkubwa wanayoifanya katika kuongeza ubunifu kwa walimu katika kufundisha wanafunzi shuleni.
Amesema Benki ya Dunia imeendelea kusaidia sekta ya elimu nchini kupitia programu mbalimbali kwa lengo la kuinua elimu ikiwemo mradi wa Heet katika vyuo vikuu na ule wa Bust kufanikisha lengo la serikali la kufikisha elimu kwa jamii.
Nae Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Elimu, Michezo na Utamaduni, Husna Sekiboko, amesema kuwa bunge la Tanzania liko pamoja na walimu katika kutetea maslahi yao hivyo hata kamati inaendea kuwatetea kuhakikisha serikali inawasaidia na kuwatetea wafanye vizuri majukumu yao.
Amesema kwa asilimia kubwa, wajumbe wa Kamati ni wabunge hivyo imechukua nafasi kubwa katika kutetea majukumu yao huku akiipomgeza Wizara ya elimu kupitia TET, kwa kufanya kazi kubwa katika kuwajari walimu.
Akizungumza kwa Niaba ya Mwenyekiti wa Baraza la TET, Prof. Joel Mtebe, amesema wameendelea kutoa mafunzo kwa walimu katika vifaa vya kufundisha na kujifunzia ili waweze kuendelea kuwa bora katika kufundisha.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Calorine Nombo amesema shindano hilo linatoa fursa ya kuimarisha ufundishaji kupitia TEHAMA, kupitia mpango wao wa kidigiti katika ufundishaji huku akiwapongeza wadau mbalimbali wa mtandao kwa kutoa ushirikiano ikiwemo kuondoa gharama kwa walimu wanao tumia MMS katika ufundishaji.
Awali Mkurugenzi Mkuu wa TET, Dkt.Aneth Komba akiwakaribisha wageni walioshiriki katika hafla hiyo, amesema usahili huo ulifanyika kwa ufanisi mkubwa na uwazi hadi kupatikana washindi kwa haki na uwazi bila upendeleo.
Amesema jumla ya kanda zilikuwa 81 zilichaguliwa na kuwasilisha ngazi ya Taifa, ambapo zilipatikana video 25 na kuwaita katika usahili ambapo walianza na video zaidi ya 3,000 na kupatikana 25, kisha washindi 10 ambao walipatiwa zawadi ya cheti na fedha kwa wakwanza hadi watatu.
Mshindi wa kwanza ni Jenipha Chuwa kutoka shule ya Enaboishu Academy ya mkoani Arusha, ambaye alipata sh. 3,000,000 na cheti, mshindi wa pili ni Sophia Moses kutoka shule hiyo hiyo ambaye alipata sh. 2,500,000 na mshindi wa tatu ni Jenister Paul kutoka shule ya Tuvalia iliyoko Meru ambaye alipata cheti na sh.2,000,000 na shindi wa nne, ni Edner kutoka shule ya Matomvu mkoani Mwanza ambaye alipata cheti na sh.500,000.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda akimpongeza na kumkabidhi hundi ya shilingi Milioni tatu (3,000,000) Mwl. Jenipha Chuwa kutoka shule ya Enaboishu Academy ya mkoani Arusha, mshindi wa kwanza wa shindano la la pili la Stadi za kufundisha somo la Kiingereza kwa shule za msingi nchini ambapo tuzo hizo ziliandaliwa na Taasisi ya Elimu Tanzania (TET). Hafla hiyo imefanyika Juni 25, 2024 katika ukumbi wa Benki ya CRDB Jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Calorine Nombo (kushoto) akimkabidhi hundi ya shilingi milioni mbili na nusu (2,500,000) Mwl. Sophia Moses kutoka shule ya Enaboishu Academy ya mkoani Arusha mshindi wa pili wa shindano la pili la Stadi za kufundisha somo la Kiingereza kwa shule za msingi nchini ambapo tuzo hizo ziliandaliwa na Taasisi ya Elimu Tanzania (TET). Hafla hiyo imefanyika Juni 25, 2024 katika ukumbi wa Benki ya CRDB Jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Calorine Nombo (kushoto) akimkabidhi hundi ya shilingi milioni mbili na nusu (2,500,000) Mwl. Sophia Moses kutoka shule ya Enaboishu Academy ya mkoani Arusha mshindi wa pili wa shindano la pili la Stadi za kufundisha somo la Kiingereza kwa shule za msingi nchini ambapo tuzo hizo ziliandaliwa na Taasisi ya Elimu Tanzania (TET). Hafla hiyo imefanyika Juni 25, 2024 katika ukumbi wa Benki ya CRDB Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda akizungumza wakati wa hafla ya ya utoaji tuzo kwa walimu walioshinda shindano la pili la Stadi za kufundisha somo la Kiingereza kwa shule za msingi nchini ambapo tuzo hizo ziliandaliwa na Taasisi ya Elimu Tanzania (TET). Hafla hiyo imefanyika Juni 25, 2024 katika ukumbi wa Benki ya CRDB Jijini Dar es Salaam
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda akizungumza wakati wa hafla ya ya utoaji tuzo kwa walimu walioshinda shindano la pili la Stadi za kufundisha somo la Kiingereza kwa shule za msingi nchini ambapo tuzo hizo ziliandaliwa na Taasisi ya Elimu Tanzania (TET). Hafla hiyo imefanyika Juni 25, 2024 katika ukumbi wa Benki ya CRDB Jijini Dar es Salaam
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda akizungumza wakati wa hafla ya ya utoaji tuzo kwa walimu walioshinda shindano la pili la Stadi za kufundisha somo la Kiingereza kwa shule za msingi nchini ambapo tuzo hizo ziliandaliwa na Taasisi ya Elimu Tanzania (TET). Hafla hiyo imefanyika Juni 25, 2024 katika ukumbi wa Benki ya CRDB Jijini Dar es Salaam
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda akizungumza wakati wa hafla ya ya utoaji tuzo kwa walimu walioshinda shindano la pili la Stadi za kufundisha somo la Kiingereza kwa shule za msingi nchini ambapo tuzo hizo ziliandaliwa na Taasisi ya Elimu Tanzania (TET). Hafla hiyo imefanyika Juni 25, 2024 katika ukumbi wa Benki ya CRDB Jijini Dar es Salaam
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Elimu, Michezo na Utamaduni, Husna Sekiboko akizungumza wakati wa hafla ya ya utoaji tuzo kwa walimu walioshinda shindano la pili la Stadi za kufundisha somo la Kiingereza kwa shule za msingi nchini ambapo tuzo hizo ziliandaliwa na Taasisi ya Elimu Tanzania (TET). Hafla hiyo imefanyika Juni 25, 2024 katika ukumbi wa Benki ya CRDB Jijini Dar es Salaam
Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Calorine Nombo akizungumza wakati wa hafla ya ya utoaji tuzo kwa walimu walioshinda shindano la pili la Stadi za kufundisha somo la Kiingereza kwa shule za msingi nchini ambapo tuzo hizo ziliandaliwa na Taasisi ya Elimu Tanzania (TET). Hafla hiyo imefanyika Juni 25, 2024 katika ukumbi wa Benki ya CRDB Jijini Dar es Salaam
Mwakilishi wa benki ya Dunia, Muna Meka akizungumza wakati wa hafla ya ya utoaji tuzo kwa walimu walioshinda shindano la pili la Stadi za kufundisha somo la Kiingereza kwa shule za msingi nchini ambapo tuzo hizo ziliandaliwa na Taasisi ya Elimu Tanzania (TET). Hafla hiyo imefanyika Juni 25, 2024 katika ukumbi wa Benki ya CRDB Jijini Dar es SalaamMkurugenzi Mkuu wa TET, Dkt.Aneth Komba akizungumza wakati wa hafla ya ya utoaji tuzo kwa walimu walioshinda shindano la pili la Stadi za kufundisha somo la Kiingereza kwa shule za msingi nchini ambapo tuzo hizo ziliandaliwa na Taasisi ya Elimu Tanzania (TET). Hafla hiyo imefanyika Juni 25, 2024 katika ukumbi wa Benki ya CRDB Jijini Dar es Salaam
Prof. Joel Mtebe akizungumza kwa niaba ya Mwenyekiti wa Baraza la TET, wakati wa hafla ya ya utoaji tuzo kwa walimu walioshinda shindano la pili la Stadi za kufundisha somo la Kiingereza kwa shule za msingi nchini ambapo tuzo hizo ziliandaliwa na Taasisi ya Elimu Tanzania (TET). Hafla hiyo imefanyika Juni 25, 2024 katika ukumbi wa Benki ya CRDB Jijini Dar es Salaam
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda akiwa pamoja viongozi wengine mbalimbali wakipata picha ya pamoja na Washindi 10 wa shindano la pili la Stadi za kufundisha somo la Kiingereza kwa shule za msingi nchini wakati wa hafla ya utoaji tuzo kwa walimu hao ambapo tuzo hizo ziliandaliwa na Taasisi ya Elimu Tanzania (TET). Hafla hiyo imefanyika Juni 25, 2024 katika ukumbi wa Benki ya CRDB Jijini Dar es Salaam
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda akiwa pamoja viongozi wengine mbalimbali wakipata picha ya pamoja na walimu ambao wameshiriki shindano la pili la Stadi za kufundisha somo la Kiingereza kwa shule za msingi nchini wakati wa hafla ya utoaji tuzo kwa walimu hao ambapo tuzo hizo ziliandaliwa na Taasisi ya Elimu Tanzania (TET). Hafla hiyo imefanyika Juni 25, 2024 katika ukumbi wa Benki ya CRDB Jijini Dar es Salaam
(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)
0 Comments