TAFITI na Ubunifu zinazoendelea kufanyika ndani ya nchi ni kutokana na msukumo wa Rais Samia kwani ameona zinatoa majibu ya changamoto mbalimbali zinazoikabili jamii ya watanzania, kama alivyotatua kero ya maji kwa wanawake kuyafuata umbali mrefu kupitia kampeni ya kumtua mama ndoo kichwani.
Ameyasema hayo leo Juni 5, 2024 Naibu Waziri wa Maji, Kundo Mathew wakati akimwakilisha Waziri wa Maji Jumaa Aweso ambaye alitarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Maadhimisho ya Tisa (9) ya Wiki ya Utafiti na Ubunifu ambayo yamefanyika katika Ukumbi wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam.
Amesema kuwa matokeo ya utafiti husaidia kupata majibu ya changamoto, na kutoa fursa kwa watanzania wengi kupata ajira na kuboresha hali za kiuchumi za watanzania wengi.
Aidha amesema mpango wa Rais Samia kupitia wizara ya maji kuleta teknolojia mpya ya kutumia mita za kisasa ( smart pre paid water meter) ili kuondoa kero ya watanzania kubambikiwa bili kubwa za maji, Upotevu wa maji kutokana na uchakavu na uzamani wa mita na kumsaidia mtanzania aweze kulipia maji kadri atumiavyo.
Pamoja na hayo Naibu Waziri Kundo ameupongeza uongozi wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam kwa kusimamia vizuri ahughuli zote za ubunifu na utafiti kwa mafanikio makubwa.
Maadhimisho hayo yebeba ujumbe huu " Kukuza utafiti na ubunifu kupitia ubia baina ya chuo kikuu cha Dar es Salaam na Tasnia mbalimbali.
0 Comments