Ticker

6/recent/ticker-posts

CHUO KIKUU MZUMBE CAU WAANZA UTEKELEZAJI WA MAKUBALIANO YA USHIRIKIANO

CHUO Kikuu Mzumbe kimepokea ugeni kutoka Chuo cha Kilimo China (CAU) ukijumuisha Wanafunzi na walimu waliowasili  kwa ajili ya programu ya kubadilishana uzoefu wa kitaaluma kwa lengo la kukuza maendeleo ya kijamii na kiuchumi ikiwa ni utekelezaji wa makubaliano ya ushirikiano baina ya vyuo hivyo viwili uliosainiwa hivi karibuni

Akizungumza wakati wa hafla ya ufunguzi rasmi wa programu hiyo iliyofanyika Julai 17,2024 kampasi kuu Morogoro , Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Prof. Allen Mushi amewakaribisha wanafunzi na walimu hao na kueleza kuwa  Wanajumuiya wote wa Chuo Kikuu Mzumbe wana furaha sana kuwapokea wana shauku kubwa katika kuendeleza ushirikiano huo baina ya vyuo hivyo viwili kwa kuwa utaendeleza uhusiano wa kihistoria wa mataifa mawili ya China na Tanzania ulioanza miongo mingi iliyopita

 “Nina imani kubwa kwamba programu hii itakuwa na manufaa makubwa kwa wote wanaoshiriki na itaacha alama ya kudumu katika maendeleo ya kijamii na kiuchumi ya mataifa yetu.” Alisema Prof. Mushi.

Awali akizungumza Mratibu wa ziara hiyo kutoka idara ya Uchumi Chuo Kikuu Mzumbe, Prof. Aurelia Kamuzora amesema ushirikiano wa vyuo hivyo ni muendelezo wa ushirikiano mzuri baina ya China na Tanzania, hivyo Chuo cha Kilimo China (CAU) wamepata fursa ya kuja Tanzania hasa Chuo kikuu Mzumbe kwa lengo la kujifunza mambo mbalimbali yakiwemo ya kijamii, utamaduni na kubadilishana uzoefu wa kitaaluma. 

Kwa upande wake mratibu wa ushirikiano huo kutoka Ndaki ya Maendeleo ya Uchumi wa Kilimo cha Kimataifa (College of International Development of Global Agricultural (CIDGA) kutoka Chuo cha Kilimo China (CAU), Prof. Tang Lixia alisema kuwa ziara yao ni fursa adhimu kwa wanafunzi wa Chuo cha Kilimo China kujifunza na kushirikiana na wenzao wa Chuo Kikuu Mzumbe.

Aidha Mkurugenzi wa Ukimaitafaji na Baraza la Wahitimu Chuo Kikuu Mzumbe, Dkt. Lucy Massoi amesema, ziara hiyo ya mafunzo ni utekelezaji wa hati ya makubaliano ya ushirikiano iliyosainiwa mwezi Oktoba 2023 baina ya vyuo hivyo viwili, hivyo ni furaha kuona makubaliano hayo yanaanza kuleta matunda yenye tija tija kwa vyuo hivyo na mataifa yao

Kwa upande wake Kaimu Naibu Mkuu wa Chuo - Taaluma Utafiti na Ushauri, Prof Eliza mwakasangula alisema, Chuo Kikuu Mzumbe kinajivunia kuwa ni Taasisi ya elimu ya juu inayotoa elimu kuanzia ngazi ya Astashahada hadi shahada ya Uzamivu na ni kitovu cha utafiti na ushauri wa kitaalamu. 

“Huduma hizi za kibobezi  zinatolewa ndani ya nchi pamoja na nje ya Tanzania kupitia programu za ushirikiano na taasisi nyingine za kitaaluma na utafiti na hivyo tuna furaha sana kuwa nanyi leo hii”
Alisema Prof. Mwakasangula

Ugeni huo kutoka Chuo cha Kilimo China CAU utakaa kwa siku saba ambapo wanafunzi hao watapata fursa ya kujifunza darasani wakisimamiwa na Wahadhiri wa Chuo Kikuu Mzumbe, kutembelea sehemu za uzalishaji pamoja na jamii ili kujifunza tamaduni za kitanzania kwa vitendo ikiwa ni sehemu ya kubadilishana uzoefu wa kitaaluma na kukuza matokeo ya utafiti baina ya vyuo hivyo.

Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Prof. Allen Mushi afungua rasmi Hafla ya Uzinduzi wa Programu ya Majira ya Joto ya Kina katika Maendeleo ya Kijamii ya Kimataifa kwa Mageuzi ya Kiuchumi.
Wanafunzi na Walimu kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo cha China (CAU) wakiwa pamoja na wenyeji wao wa Chuo Kikuu Mzumbe baada ya Uzinduzi rasmi wa Programu ya Majira ya Joto ya Kina katika Maendeleo ya Kijamii ya Kimataifa kwa Mageuzi ya Kiuchumi.
Kaimu Makamu wa Chuo Kikuu Mzumbe Prof. Allen Mushi (kulia) akizungumza na Prof. Zhang Yue (kushoto) na prof. Tang Lixia (katikati) wa Chuo Kikuu cha Kilimo cha China (CAU) waliowasili chuoni hapo kwa ajili ya Programu ya Majira ya Joto ya Kina katika Maendeleo ya Kijamii ya Kimataifa kwa Mageuzi ya Kiuchumi.
Mfawidhi (MC) wa Hafla ya Uzinduzi wa Programu ya Majira ya Joto ya Kina katika Maendeleo ya Kijamii ya Kimataifa kwa Mageuzi ya Kiuchumi Bw. Kelvin Mwita akiongoza zoezi la utambulisho na itifaki ya viongozi waliohudhuria hafla hiyo.
Mratibu wa Mahusiano kati ya Chuo Kikuu Mzumbe na Chuo Kikuu cha Kilimo cha China (CAU) Prof. Aurelia Kamuzora akitoa neno la utangulizi katika Hafla ya Uzinduzi wa Programu ya Majira ya Joto ya Kina katika Maendeleo ya Kijamii ya Kimataifa kwa Mageuzi ya Kiuchumi
Mtiva wa Kitivo cha Sayansi za Jamii Chuo Kikuu Mzumbe Dkt. Harold Utouh akielezea manufaa ya Programu ya Majira ya Joto ya Kina katika Maendeleo ya Kijamii ya Kimataifa kwa Mageuzi ya Kiuchumi katika hafla ya uzinduzi wa programu hiyo.
Kaimu Naibu Makamu Mkuu wa chuo - Taaluma, Utafiti na Ushauri Prof. Eliza Mwakasangula akielezea kuhusu Chuo Kikuu Mzumbe kwa wageni kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo cha China (CAU) katika Hafla ya Uzinduzi wa Programu ya Majira ya Joto ya Kina katika Maendeleo ya Kijamii ya Kimataifa kwa Mageuzi ya Kiuchumi.
Mkurugenzi wa Ukimataifaji na Baraza la Wahitimu Chuo Kikuu Mzumbe Dkt. Lucy Massoi akielezea kuhusu ushirikiano katika ya Chuo Kikuu Mzumbe na Chuo Kikuu cha Kilimo cha China (CAU) katika Hafla ya Uzinduzi wa Programu ya Majira ya Joto ya Kina katika Maendeleo ya Kijamii ya Kimataifa kwa Mageuzi ya Kiuchumi.
Baadhi ya Washiriki wakiwemo Wageni kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo cha China, Wanafunzi na Wahadhiri kutoka Chuo Kikuu Mzumbe wakisikiliza kwa makini baadhi ya mawasilisho katika Hafla ya Uzinduzi wa Programu ya Majira ya Joto ya Kina katika Maendeleo ya Kijamii ya Kimataifa kwa Mageuzi ya Kiuchumi.
Picha ya Pamoja ikihusisha baadhi ya Wajumbe wa Menejimenti ya Chuo Kikuu Mzumbe, Wanafunzi na Wahadhiri wa Chuo Kikuu Mzumbe na Wageni kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo cha China (CAU) baada ya Hafla ya Uzinduzi wa Programu ya Majira ya Joto ya Kina katika Maendeleo ya Kijamii ya Kimataifa kwa Mageuzi ya Kiuchumi

Post a Comment

0 Comments