Ticker

6/recent/ticker-posts

EWURA YAENDELEA KUTOA ELIMU KWENYE MAONESHO SABASABA

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

SERIKALI kupitia Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imesema kuwa itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali katika kuhamasisha matumuzi ya nishati safi ya kupikia ili kuendana na Mkakati wa Kitaifa ambao umelenga kuhakikisha Watanzania wanahamia kwenye matumizi ya nishati safi ya kupikia.

Hayo yamebainishwa katika viwanja vya maonesho ya 48 ya biashara kimataifa 7 7 na Meneja mawasiliano na uhusiano –EWURA Titus Kaguo wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ushiriki wao katika maonesho hayo.

Katika hatua nyingine Kaguo amesema serikali itaendelea kuhamasisha matumizi ya gesi asilia katika vyombo vya moto ikiwemo magari ili kuendeleza matumizi ya nishati safi huku wito ukitolewa kwa wawekezaji kujikita katika uwekezaji wa vituo vya gesi hiyo –CNG.

"Tunawahamasisha wawekezaji wawekeze kwenye vituo vya ujazaji wa gesi asilia ambapo utaratibu umesharekebishwa na TBS kwamba kituo cha mafuta kinaweza kuwa kinauza gesi asili kwenye magari". Amesema Kaguo.

Pamoja na mambo mengine Kaguo amesema –EWURA imekusudia kutumia maonesho hayo katika kutoa elimu kuhusu huduma mbalimbali zinatolewa na mamlaka hiyo.

Amesema kupitia Maonesho hayo imekuwa fursa kukutana na wadau pamoja na wananchi kwa ujumla kutoa elimu kuhusu masuala ya petroli, umeme, gesi asilia pamoja na maji na usafi wa mazingira.

Post a Comment

0 Comments