Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda amesema ni muhimu kufanya utafiti wa kisayansi kusaidia kukwamua changamoto za uzalishaji sekta mbalimbali ikiwemo Elimu na kilimo kuchochea ustawi Endelevu wa maendeleo kiuchumi.
Mkenda amesema hayo leo Julai 10, 2024 jijini Dar es Salaam wakati akizungumza katika Ufunguzi wa Mkutano Mkuu unaojadili ushahidi wa matokeo ya tafiti, ambapo amesisitiza kufanyia tathimini ya mara kwa mara Sera zinazotungwa na kutekeleza ili kuleta mabadiliko yanayokusudiwa ya muda mrefu.
Aidha Mkenda amewahimiza Watafiti kuwa wakati wa kufanya tathimini ni muhimu kuzingatia mambo makuu matatu moja kuangalia mwenendo wa idadi ya watu katika nchi, ili kuwa na mipango mizuri na yenye manufaa kwa Taifa, hivyo tafiti zinapaswa kusaidia kutatua changamoto zinazokabili makundi mbalimbali ikiwemo Wazee na Vijana kwa kuzingatia kipaumbele vyao.
Pia amewataka Wataalamu wa uchumi na wadau wa maendeleo kuisaidia jamii kutumia teknolojia kwa manufaa chanya pamoja na kukabiliana na mabadiliko hayo.
0 Comments