Ticker

6/recent/ticker-posts

NAIBU WAZIRI NYONGO- MAONESHO SABASABA NI FURSA KUTANGAZA NA KUWAKARIBISHA WAWEKEZAJI NCHINI

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji Mhe. Stanslaus Nyongo (Mb.) amesema Maonesho ya 48 ya Kimataifa ya Biashara maarufu (Sabasaba) ni fursa muhimu ya kutangaza na kuwakaribisha wawekezaji ili kuona fursa mbalimbali za uwekezaji nchini.

Ameyasema hayo leo tarehe 03 Julai, 2024 katika mahojiano maalumu aliyofanya baada ya kutembelea Taasisi zilizo chini ya Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji zilizoshiriki maonesho ya Sabasaba.

Ameongeza kuwa Maonesho hayo yamekuwa na mvuto mkubwa kwa kuwa Wizara na Taasisi zilizoshiriki zimeonesha fursa zilizopo katika uwekezaji.

"Tanzania tunaona hii ni fursa nzuri ya kujitangaza kama nchi na kukaribisha wawekezaji mbalimbali kuona fursa za uwekezaji katika nchi yetu" amesema Mhe.Nyongo

Aidha, amepongeza namna ambavyo wafanyabishara wamekuwa wabunifu na makampuni ya nje yaliyokuja kuonesha shughuli za uwekezaji wanazoweza kufanya nchini.

Post a Comment

0 Comments