Ticker

6/recent/ticker-posts

NIDA YAWATAKA WENYE VITAMBULISHO VILIVYOFUTIKA KUVIREJESHA

MAMLAKA ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) imewataka wananchi wote ambao vitambulisho vyao vimepata hitilafu ya kufutika maandishi kuvirejesha katika ofisi za NIDA ama katika ofisi za Serikali za Mitaa, Kata, Vijiji na Shehia ambako vitakusanywa na kurejeshwa kwa ajili ya kuchapishwa upya bila malipo yeyote kwa mwananchi.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa Idara ya Vitambulisho kutoka NIDA Edson Guyai wamepokea taarifa ya kuwepo kwa Vitambulisho vichache kufutika taarifa zailizochapwa mbele au nyuma ya kitambulisho mfano majina, picha au Namba ya Kitambulisho au tarehe ya kuzaliwa.

Mkurugenzi huyo amesema takwimu za Mamlaka hiyo zinaonyesha kuwa vitambulisho vyenye hitilafu hiyo ni 21,224 sawa na asilimia 0.09 ya vitambulisho 21, 32,098 viliyozalishwa.

Ametoa rai kwa mwananchi ambaye Kitambulisho chake kitakuwa na changamoto hiyo akirudishe ofisi ya NIDA au kwa mtendaji alipokichukua ili virudishwe na kuchapishwa upya.

Amesema kumekuwa na upotoshaji kuhusu ubora wa vitambulisho vya Taifa kutokana na changamoto hiyo ndogo iliyojitokeza na amesisitiza kwamba Vitambulisho vya Taifa vinavyotolewa na Mamlaka hiyo vina ubora unakidhi viwango vya kimataifa.

Amedokeza kuwa kwa sasa wataalamu wanaendelea na uchunguzi kubaini chanzo cha tatizo hilo kama ni mashine, wino au kadi. Hii itawezesha kufidiwa kwa kadi hizo kama yalivyo matakwa ya mkataba bila Serikali kuingia gharama yeyote.

Mkurugenzi huyo amesema hitilafu ndogondogo ni jambo la kawaida kutokea katika sekta ya uzalisha wa bidhaa duniani huku akieleza kuwa hata kammpuni kubwa za uzalishaji kama magari na simu za mkononi hupata changamoto kama hizi.
Mwananchi akichukuliwa alama za vidole katika moja ya ofisi za NIDA kwa ajili ya Utambulisho wake wa Taifa.

Mwananchi akipigwa picha kwa ajili ya utambulisho wa Taifa.
Mwananchi akikabdhiwa Kitambulisho chake katika moja ya ofisi za Serikali ya Mtaa

Post a Comment

0 Comments