Ticker

6/recent/ticker-posts

OFISI YA MSAJILI YAENDESHA MAFUNZO KWA VIONGOZI WA VYAMA VYA SIASA

MSAJILI wa Vyama Vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi amevitaka Vyama Vya Siasa kuepuka migogoro ambayo imekuwa ikijitokeza kwenye vyama hivyo kwani kunaweza kusababisha kuleta mifarakano katika taifa.

Agizo hilo amelitoa leo Julai 9,2024 jijini Dar es Salaam wakati akifungua mafunzo ya siku mbili kwa viongozi wa vyama vya siasa nchini yakiwa na lengo la kuwajengea uwezo juu ya  mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji wa vyama hivyo pamoja na namna ya kuhimili migogoro inayotokea wenyewe kwa wenyewe pasipo kufikishana ngazi za juu.

 Jaji Mutungi amesema vyama vya siasa ni Taasisi hivyo vinapaswa kusajiliwa na kutenda Majukumu yanayotambulika kidemokrasia na kuachana na vurugu ambazo zinasababisha vyama hivyo kuwa na mpasuko.

Aidha, amevitaka vyama vya siasa kuwa vinara wa kujenga nchi na kwamba Tanzania sio nchi ambayo inapata utawala kwa mabavu bali ni demokrasia iliotukuka.

 “Mkifanya maovu hakuna atakaewafuata, nitoe wito kwenu viomgozi muwambie wafuasi wenu waepukanae na migogoro yasiyo ya lazima na badala yake walinde amani na utulivu wa Taifa tulionao toka zamani hadi sasa”amesema Jaji Mutungi

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Chama Cha ACT - Wazalendo Ado Shaibu amesema kuwa migogoro ya vyama vya siasa inapaswa kutatuliwa kwa njia ya maridhiano na sio kutumia nguvu zisizofaa.

 "Tunaishukuru ofisi ya msajili wa vyama vya siasa kutuletea mafunzo haya kwani yanakwenda kutupunguzia namna ya kuepuka migogoro ambayo imekuwa ikitokea mara kwa mara ndani ya vyama vyetu" amesema Shaibu 

Naye, Mwenyekiti Taifa wa Chama cha Demokratic Party (DP) Philipo Fumbo amesema vyama vingi vya upinzani havina ruzuku kutoka serikalini hali ambayo inachangia kushindwa kuajiri wahasibu na maafisa ununuzi nakupelekea migogoro ndani ya vyama kutokana na matumizi mabaya ya fedha.
Msajili wa Vyama Vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi akizungumza wakati akifungua Mafunzo ya Siku mbili kwa Viongozi wa Vyama Vya Siasa nchini kwa lengo la kuwajengea uwezo juu ya  mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji wa vyama hivyo pamoja na namna ya kuhimili migogoro inayotokea wenyewe kwa wenyewe pasipo kufikishana ngazi za juu. Mafunzo hayo yamefunguliwa leo Julai 9,2024 jijini Dar es Salaam

Baadhi ya viongozi wa Vyama vya siasa nchini wakiwa kwenye mafunzo ya siku mbili yanayolenga kuwajengea uwezo juu ya  mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji wa vyama hivyo pamoja na namna ya kuhimili migogoro inayotokea wenyewe kwa wenyewe pasipo kufikishana ngazi za juu. Mafunzo hayo ni ya siku mbili ambapo yamefunguliwa leo Julai 9,2024 jijini Dar es Salaam na  Msajili wa Vyama Vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi.

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

Post a Comment

0 Comments