Ticker

6/recent/ticker-posts

WAZIRI JAFO APONGEZA UWEKEZAJI KIWANDA CHA SUKARI KILOMBERO


Waziri wa Viwanda na Biashara, Dkt. Selemani Jafo,akikagua kiwanda cha sukari Kilombero kilichopo mkoani Morogoro mara baada ya kutembelea kiwanda hicho leo Julai 31,2024.

Na Mwandishi Wetu, MOROGORO

Waziri wa Viwanda na Biashara, Dkt. Selemani Jafo leo ameupongeza uongozi wa kiwanda cha sukari Kilombero kilichopo mkoani Morogoro kwa uwekezaji mkubwa na kwasasa kinafanyiwa upanuzi mkubwa wa gharama ya sh. Bilioni 650.

Uwekezaji huo utaongeza uwezo wa uzalishaji wa sukari kutoka Tani 130,000 za sasa hadi Tani 270,000 na hivyo kuchangia kuondoa upungufu wa sukari hapa nchini.

Akizungumza Julai 31, 2024 alipotembelea kiwanda hicho, Waziri Jafo amekipongeza pia kiwanda hicho kwa kuchangia upatikani wa ajira hapa nchini.

"kwasasa kiwanda hicho kimeajiri wafanyakazi 4500 huku wakulima 11,000 wamewezeshwa na wanauza miwa yao kiwandani hapo na mapato yanayokwenda kwa wakulima hao ni wastani wa sh. bilioni 67 kwa mwaka."amesema Dkt.Jafo

Dkt. Jafo amewahakikisha wawekezaji wote hapa nchini kwamba serikali ya Dkt. Samia Suluhu Hassan inawapongeza wawekezaji wote na itaendelea kulinda uwekezaji wa viwanda vya aina mbalimbali vilivyopo hapa nchini kwa lengo kukuza uchumi na kulinda ajira za watanzania.


Waziri wa Viwanda na Biashara, Dkt. Selemani Jafo,akikagua kiwanda cha sukari Kilombero kilichopo mkoani Morogoro mara baada ya kutembelea kiwanda hicho leo Julai 31,2024.


Waziri wa Viwanda na Biashara, Dkt. Selemani Jafo,wakipata Maelezo mara baada ya kukagua kiwanda cha sukari Kilombero kilichopo mkoani Morogoro mara baada ya kutembelea kiwanda hicho leo Julai 31,2024.


Waziri wa Viwanda na Biashara, Dkt. Selemani Jafo, aakizungumza mara baada ya kukagua kiwanda cha sukari Kilombero kilichopo mkoani Morogoro mara baada ya kutembelea kiwanda hicho leo Julai 31,2024.

Post a Comment

0 Comments