Ticker

6/recent/ticker-posts

WAZIRI NDEJEMBI AKUTANA NA WARATIBU WA MIRADI YA WIZARA YA ARDHI

Na Mwandishi Wetu

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Deogratius Ndejembi amekutana na waratibu wa miradi inayotekelezwa na wizara yake makao makuu ya wizara eneo la Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma tarehe 31 Julai 2024.

Waratibu aliokutana nao ni wale wanaotekeleza Miradi wa Uboreshaji Usalama wa Milki za Ardhi nchini (LTIP), Mradi wa Uwekeji Miundombinu ya Upimaji (LDI) pamoja na mradi wa Kupanga, Kupima na Kumilikisha Ardhi (KKK)

Akizungumza katika kikao hicho, Mhe, Ndejembi amesema uamuzi wa kukutana na waratibu wa miradi kwanza ni kupata ufahamu wa miradi inayotekelezwa na wizara kabla ya kuanza kwa vikao vya kamati za Bunge mapema mwezi Agosti 2024.

Mhe. Ndejembi aliteuliwa kushika wadhifa wa Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi hivi karibuni akichukua nafasi ya Mhe. Jerry Silaa aliyehamishiwa wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Deogratius Ndejembi akizungumza wakati wa kikao chake na waratibu wa miradi inayotekelezwa na wizara ya Ardhi katika ofisi za Wizara Mtumba jijini Dodoma tarehe 31 Julai 2024.
Mkurugenzi wa Upimaji na Ramani Hamdouny Mansoor akizungumza kwenye kikao baina ya Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Deogratius Ndejembi na waratibu wa miradi inayotekelezwa na wizara ya ardhi tarehe 31 Julai 2024 jijini Dodoma.
Mratibu wa Mradi wa Ubireshaji Usalama wa Milki za Ardhi (LTIP) Joseph Shewiyo akielezea utekelezaji mradi wa LTIP mbele ya Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Deogratius Ndejembi alipokutana na waratibu wa miradi kwenye ofisi za wizara Mtumba jijini Dar es Salaam tarehe 31 Julai 2024.
Sehemu ya Maafisa wa Wizara ya Ardhi wakiwa katika kikao na Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Deogratius Ndejembi alipokutana na waratibu wa miradi ya wizara ya ardhi katika ofisi ya wizara Mtumba jijini Dodoma tarehe 31 Julai 2024 (PICHA ZOTE NA WIZARA YA ARDHI)

Post a Comment

0 Comments