Ticker

6/recent/ticker-posts

PROF. MWEGOHA AELEZEA MCHANGO WA SEKTA YA ELIMU KATIKA SHUGHULI ZA KILIMO

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Prof. William Mwegoha ameelezea Mchango wa Sekta ya Elimu ya juu katika kuimarisha sekta ya Kilimo katika maendekeo endelevu. Prof. Mwegoha amefafanua hayo leo katika mahojiano ya moja kwa moja kupitia EFM na TVE Tanzania kupitia kipindi cha Joto la Asubuhi leo tarehe 08 Agosti 2024.

Aidha Prof. Mwegoha ametumia nafasi hiyo kueleza namna Chuo Kikuu Mzumbe kinavyojihusisha na shughuli za kilimo kupitia miradi mbalimbali ya utafiti pamoja na ushirikiano wa moja kwa moja na taasisi nyingine za kilimo ndani na nje ya nchi.

Vilevile ameeleza juu ya mpango wa matumizi ya ardhi ya Chuo Kikuu Mzumbe kwa ajili ya shughuli mbalimbali za maendeleo ikiwemo ujenzi wa miundombinu na kilimo chenye tija.

Karibu Chuo Kikuu Mzumbe, “Tujifunze kwa Maendeleo ya Watu”

Post a Comment

0 Comments