KAMPUNI
ya Vodacom Tanzania kwa kushirikiana na Kampuni ya Huawei Tanzania
wamezindua darasa ya kidigitali inayoitwaa digi truck, ambapo Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amezindua kama mgeni rasmi.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo leo Agosti
24, 2024 amesema serikali itaendelea kutoa kipaumbele katika matumizi
ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano ili iweze kuwa na mchango mkubwa
katika maendeleo ya kiuchumi kama inavyoelekezwa katika Dira ya Taifa ya
2025, Sera ya Maendeleo ya TEHAMA ya mwaka 2016 na Ilani ya CCM
2020-2025.
Amesema
kuwa, Serikali inahamasisha matumizi ya TEHAMA ili kuwezesha wananchi
hususani vijana na kizazi kijacho kushindana katika uchumi wa dunia.
"Kwa
kuimarisha elimu ya TEHAMA, tunajenga jamii yenye ujuzi wa kutumia
teknolojia kwa ufanisi, kubuni suluhisho za ubunifu, na kuchangia katika
uchumi wa kidijitali. Hii itasaidia katika kuhakikisha kwamba maendeleo
ya kidijitali yanakutanisha kila mmoja, bila kujali hali ya kiuchumi."
Amesema Dkt. Biteko.
Ameongeza
kuwa, Serikali inayoongozwa na Rais Samia itafanya kila linalowezekana
kuhakikisha kwamba wawekezaji wanakuwa msaada katika kubadilisha hali
maisha ya watu kupitia nyanja mbalimbali ikiwemo TEHAMA huku pia
wawekezaji hao wakinufaika na uwekezaji wao.
Dkt.
Biteko amesema uchumi wa kidijitali ni muhimu katika kuleta maendeleo
kwa kuongeza ufanisi katika uzalishaji na na kuleta fursa na mapato ya
ziada kwa wananchi.
Kwa
upande wake, Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari,
Mhe. Jerry Silaa amewapongeza Huawei na Vodacom kwa kuja na teknolojia
ya Digi Truck ambayo inakwenda kuwa msaada kwa vijana wengi nchini
ambayo itafika kila sehemu ili vijana wengi wajifunze.
Teknolojia
hiyo iliyozinduliwa leo kutoka kampuni ya Vodacom Tanzania na Huawei
itawezesha wananchi kupata elimu na ujuzi wa TEHAMA.
Nae
Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Vodacom Tanzania, Philip Besiimire amesema
Mpango huo unalenga kuwapatia Watanzania ujuzi wa msingi wa kidijitali
na kuwaboreshea ujuzi na maarifa, ukilenga wanafunzi zaidi ya 5,500,
wanawake, na vijana katika mikoa 10 kila mwaka kwa kipindi cha miaka 3
ijayo.
Aidha
amesema kuwa Programu hiyo itatoa uzoefu wa kujifunza wa kubadilisha
maisha kupitia vipindi viwili maalum, ambapo kuna Programu ya siku 6
katika shule za sekondari kwa vijana wa umri wa miaka 16 hadi 19, na
Programu ya wiki 2 kwa vijana waliojiajiri na wanawake wajasiriamali wenye umri wa miaka 20 na kuendelea.
Amesema
Darasa hilo la kidijitali linalotembea linaonesha kujitolea kwao
kuwawezesha Watanzania kupata ujuzi muhimu wa kidijitali, hususani kwa
maeneo na watu walio na upungufu wa fursa.
"Kupitia
programu maalum kwa shule za sekondari, vijana waliojiajiri, na
wanawake wajasiriamali, DigiTruck inalenga kuwawezesha Watanzania na
nyenzo wanazohitaji ili kufanikiwa katika ulimwengu unaozidi kuwa wa
kidijitali". Amesema
Naibu Waziri Mkuu na Waziri Wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko (wa nne kulia) akikata utepe kama ishara ya Uzinduzi wa Mpango wa Ujuzi wa Kidigitali kwa Wote (DigiTruck) tukio lililofanyika leo Agosti 24,2024 katika ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC), Jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri Mkuu na Waziri Wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa Mpango wa Ujuzi wa Kidigitali kwa Wote (DigiTruck) tukio uliofanyika leo Agosti 24,2024 katika ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC), Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Jerry Silaa akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa Mpango wa Ujuzi wa Kidigitali kwa Wote (DigiTruck) tukio uliofanyika leo Agosti 24,2024 katika ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC), Jijini Dar es Salaam.
Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Vodacom Tanzania, Philip Besiimire akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa Mpango wa Ujuzi wa Kidigitali kwa Wote (DigiTruck) tukio uliofanyika leo Agosti 24,2024 katika ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC), Jijini Dar es Salaam.
Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Huawei, Damon zhang akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa Mpango wa Ujuzi wa Kidigitali kwa Wote (DigiTruck) tukio uliofanyika leo Agosti 24,2024 katika ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC), Jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Doto Biteko akimfurahia Mwanafunzi wa Darasa la sita, Jasmine Ali kutoka Shule ya Msingi Oysterbay baada ya kumpisha Mimbari kwa ajili ya kuwasilisha shukrani kwa nimba ya Wanafunzi walioshuhudia Uzinduzi wa Mpango wa Ujuzi wa kidigitali kwa wote (DigiTruck), Tarehe 24, Agosti 2024, Jijini Dar es Salaam.
0 Comments