Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Exaud Kigahe,akitoa maelekezo baada ya kutembelea kituo Cha Forodha cha Tarakea kilichopo Wilaya ya Rombo Mkoa wa Kilimanjaro kwa ya ziara ya kukagua shughuli zote za kibiashara zinazofanyika katika mipaka yote ya Mikoa ya kaskazini
.........
Naibu waziri wa Viwanda na Biashara Mhe.Exaud Kigahe Amesema kuwa Serikali itaendelea kuweka mazingira rafiki kwa wafanyabiashara wa mipakani ili mitaji yao ikue kutoka midogo kuwa katika wastani wa wafanyabiashara wakubwa.
Mhe. Kigahe ameyasema hayo leo septemba ,2024 alipokuwa akiongea na menejimenti ya wafanayakazi wa kituo Cha forodha cha Tarakea na wawakilishi wa wafanyabiashara wilayani Rombo Mkoani Kilimanjaro.
Aidha mesema kuwa, Serikali kupitia Wizara ya Viwanda na Biashara lengo lake ni kuwafanya wafanyabiashara wetu waweze kuuza bidhaa za mwisho watoke kwenye utaratibu wa kuuza Mazao na malighafi
Ameeleza kuwa Elimu ya ulipaji kodi iendelee kutolewa maafisa wa TRA ili kutanua wigo wa ulipaji kodi kusudi fedha itakayokusanywa iweze kuleta Maendeleo ikiwemo barabara,hospitali,shule na Masoko.
Nae Meneja wa TRA Mkoa wa Kilimanjaro Bw.James Jilala ameeleze kuwa Tarekea ni moja ya vituo vinavyokua kwa kasi sana katika kuchangia mapato ya Serikali.
Kwa upande wake Alexander Mpwagi Afisa Mfawidhi wa Forodha wa Tarakea ,akisoma taarifa ya utekelezaji wa kituo hicho ,amesema kuwa kituo kina ujumla wake kina watumishi 14 wanaotoka katika taasisi tofauti tofauti.
Kuhusu makusanyo ya mapato ya forodha ameeleza kuwa Mwaka 2023-2024 lengo likuwa kukusanya 24.5 Bilioni , makusanyo halisi yaliyopatikana ni 22.Bilioni
Aidha kwa mwaka 2024 kwa kipindi cha mwezi Januari hadi Agosti kiasi Cha Shilingi 16.4 zimekusanywa.
Amezitaja bidhaa zinazoingia katika mpaka wa Tarakea kutoka nchi jirani ya Kenya ni Sabuni,Chewing gum,Margarine,Pipi na Food grade.
Kwa upande wa bidhaa zinazosafirshwa kutoka Tanzania kwenda Kenya kupitia mpaka wa Tarakea ni Makaa ya Mawe,Liquilified Petroleum gas,na bidhaa za mazo kama machungwa,Vitunguu,maji,Karanga,Viazi, na Mahindi.
Nae Katibu wa wafanya Biashara Wilaya ya Rombo Bw. Joseph Masika ameeleza changamoto zinazowakabili wafanyabiashara wa Biashara kutokuwa na magahala ya kuhifadhia mazao pindi wanapomaliza kuyavuna shambani.
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe.Exaud Kigahe akisalimiana na Mhe. Nurdin Babu Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake ya kikazi ya kutembelea mipaka iliyopo Mikoa ya Kaskazini ikiwemo Tarakea na Holili.
Naibu Waziri w Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kigahe akisaini kitabu Cha wageni baada ya kuwasili katika Ofisi Mkuu wa Wilaya ya Rombo Kwa ajili ya ziara yake ya kikazi ya kutembelea mipaka yote iliyopo katika Mikoa ya kaskazini . anatembelea Mpaka wa Tarakea na Holili.
Mkuu wa Wilaya ya Rombo Mhe.Reimond Mwangala akifanya utambulisho wa watumishi anaofanya nao kazi katika Ofisi yake kwa Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kigahe mara baada ya kuwasilia katika Wilaya hiyo kuanza ziara ya kutembelea mipaka ya Tarakea na Holili Mkoani Kilimanjaro.
Meneja wa Mfawidhi wa Kituo Cha forodha cha Tarakea Bw. Alexander Mpwagi akisoma taarifa ya utendaji wa kituo hicho kwa Mhe Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kigahe baada ya ziara yake kituoni hapo yenye lengo la kukagua shughuli za Biashara katika zinazoendeshwa katika vituo vyote vya mipakani Mikoa ya Kaskazini.
0 Comments