Ticker

6/recent/ticker-posts

BARABARA YA LAMI YA KM 7.7 YENYE THAMANI YA BILIONI 9.3 KUUNGANISHA MIKOA YA SINGIDA-SIMIYU-ARUSHA


Wakazi wa Wilaya ya Iramba na Mkalama, Mkoani Singida, wanatarajia kunufaika na barabara ya kiwango cha lami inayojengwa kuunganisha mikoa ya Singida, Simiyu, hadi Arusha. Mradi huu, wenye thamani ya shilingi bilioni tisa, umefikia asilimia 65 ya utekelezaji.

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Jerry Silaa, ametembelea na kukagua mradi huo ambao ukikamilika utawasaidia wananchi katika usafirishaji wa mazao ya kilimo, hivyo kuimarisha biashara.

Amesema ameridhishwa na kasi ya utekelezaji wa mradi huo unaoonesha namna Serikali inavyofanya kazi kubwa ya kutekeleza mradi ya maendeleo kwa ajili ya kuboresha maisha ya wananchi wake bila ubabaishaji.

Meneja wa Wakala wa Barabara (Tanroads) Mkoani Singida, Msama Msama, alieleza kuwa kipande cha barabara kinachojengwa kati ya Kitukutu-Gumanga-Mkalama na Chemchem-Sibiti, kikiwemo Kitukutu-Kinampanda, chenye urefu wa kilomita 7.7, kitagharimu bilioni 9.31 na kinajengwa na mkandarasi mzawa.

“RAIS SAMIA NA MAENDELEO, WASIKIE NA WAONE”.

Post a Comment

0 Comments