NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
Kuelekea Siku ya Mtoto wa Kike Duniani Oktoba 11,2024 wanaharakati wa masuala ya jinsia,wameiomba jamii kutambua uwezo alionao mtoto wa kike kwani anaweza kuongoza na kufanya mambo mengine kama ilivyo kwa mtoto wa kiume endapo Jamii itamthamini na kumpa kipaumbele.
Wamesisitiza kuwa watoto wa kike wana uwezo mkubwa wa kufanikiwa wakipatiwa ulinzi, upendo, na elimu stahiki.
Akizungumza leo Oktoba 9, 2024 katika semina za Jinsia na Maendeleo (GDSS) Mwezeshaji Prisca Bryson amesema mtoto wa kike ni mtu ambaye anachangamoto nyingi na kutokana na mtazamo wa jamii hana mahali pakusema
"Hana pakulia asikilizwi, haonekani, na kila mtu anathamini mtoto wa kiume zaidi," amesema Prisca.
Kwa upande wake Mdau wa Semina za Jinsia na Maendeleo, Austin Mwakibete amesema kuwa elimu ya kijinsia na darasani ni muhimu kwa watoto wa kike, na akasisitiza umuhimu wa kuwashirikisha katika maamuzi yanayowahusu.
"Kuhusisha watoto wa kike katika maamuzi kutasaidia kupunguza ndoa za utotoni, na hivyo kuimarisha nafasi yao katika jamii". Amesema
Hizi ni juhudi muhimu za kuhamasisha jamii kutambua uwezo na thamani ya mtoto wa kike, ili waweze kukua katika mazingira salama na yenye fursa sawa.
0 Comments