Mjumbe wa Kamati kuu ya CCM Taifa na Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana UVCCM Ndg. Mohammed Ali Kawaida amesema moja ya sababu inayopelekea kusuasua kwa zoezi la uandikishaji la wapiga kura kwenye daftari la Makaazi Mkoani Kagera ni pamoja na zoezi la uboreshaji wa daftari la kudumu la NEC pamoja na usajili wa wanachama wa CCM.
Kawaida ametoa ufafanuzi na elimu hiyo wakati wa ziara yake wilayani Muleba alipokutana na kuzungumza na wananchi katika maeneo mbalimbali leo Oktoba 18, Mwaka huu ukiwa ni mwendelezo wa ziara yake mkoani Kagera yenye lengo la kuhamasisha uandikishaji wa wapiga Kura.
Akiongea katika kata za Runazi, Rulanda na Muleba Mjini, @comrade_kawaida amewataka wananchi kutofautisha uandikishaji huu wa makaazi na uandikishaji uliopita sambamba na kuwataka viongozi katika mikoa ambayo uandikishaji upo chini kutumia siku zilizobaki kutoa elimu kwa wananchi.
Hata hivyo Kawaida ameenedelea kuwahimiza wananchi ambao hawajajiandikisha kuendelea kutumia siku zilizobaki kujiandikisha ili kuweza kupata sifa za kupiga kura na kuwachagua viongozi bora watakao waongoza katika serikali za vijiji, Vitongoji na mitaa pamoja na wajumbe wao.
0 Comments