Ticker

6/recent/ticker-posts

TET NA TEZ zaingia makubaliano ya kiutendaji kwa lengo la kukuza elimu.

Taasisi ya Elimu Tanzaia(TET) na Taasisi ya Elimu Zanzibar(TEZ) leo tarehe 11/10/2024 zimesaini hati mbili za makubaliano ya kiutendaji kwenye eneo la vifaa vya kufundishia na kujifunzia ambapo lengo kuu ni kuweka ushirikiano kwa pande zote mbili katika kukuza suala la elimu .

Makubaliano hayo yamesainiwa na wakurugenzi wakuu wa Taasisi hizo ambapo kwa upande wa TET , aliyesaini alikuwa Mkurugenzi Mkuu Dkt. Aneth Komba na upande wa TEZ makubaliano yamesainiwa na Mkurugenzi Mkuu ,Bw.Abdallah Mohamed Musa

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali ,Zanzibar Bw. Khalid Masoud Waziri ambaye alikuwa shuhuda katika hafla hiyo ya utiaji Saini ,amezitaka pande zote mbili kufanya ushirikiano mzuri wenye lengo la kuinua elimu katika maeneo yote.

“Hili ni jambo kubwa na jema lenye lengo la kuinua elimu katika maeneo yetu, hivyo naomba mshirikiane vizuri mbadilishane wataalamu katika kuhakikisha makubaliano mliyoyafikia yanaleta tija katika suala la elimu”amesema Bw.Waziri.

Kwa upande wake ,Mkurugenzi Mkuu wa TET, Dkt. Aneth Komba amesema kuwa hati ya kwanza ni ya ushirikiano katika uchapaji wa vitabu vya Elimu ya Sekondari vilivyoandaliwa kwa kufuata mtaala ulioboreshwa wa 2023 na lengo kuu likiwa ni kuongeza ushiriki wa pande zote mbili katika kuchapa na kusambaza vitabu vya elimu ya sekondari kwa wakati ili viweze kupatikana katika pande zote za nchi kabla ya muda wa utekelezaji wa mtaala kuanza kwa vidato husika.

Aidha, Dkt. Komba ameeleza kuwa hati ya pili inahusu uandishi wa vitabu vya elimu ngazi ya Maandalizi na Elimu ya Msingi ambapo ,ushirikiano huo unalenga kuunganisha nguvu kazi, utaalamu na uzoefu ili kuandaa vitabu vyenye ubora unaostahili kwaajili ya wanafunzi wetu wa ngazi hiyo ya elimu.

“Ni matumaini yangu kuwa ushirikiano huu utaongeza tija zaidi katika utoaji wa elimu iliyo bora katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania”amesema Dkt. Komba.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa TEZ , Bw.Abdallah Mohamed Mussa amesema kuwa ushirikiano huo utawezesha katika ukuaaji wa limu Zanzibara kutokana na makubaliano hayo .

“Hakika huu ni ushirkkiano bora wenye lengo jema kwenye elimu kwa pande zote mbilli na kuwa tutahakikisha tunafanya kazi kwa weledi na kubadilishana uzoefu katika kufanya kazi zote zilizopo kwenye makubalino hayo”amesema, Bw. Musa.

Post a Comment

0 Comments