Ticker

6/recent/ticker-posts

UJENZI WA SHULE YA SEKOUTOURE WAPUNGUZA MSONGAMANO WA WANAFUNZI ILONGERO


Waziri Habari, Mawasiliano na Teknilojia ya Habari, Mhe. Jerry William Silaa ameweka jiwe la msingi Shule Mpya ya Sekondari Sekoutoure iloyopo Kata ya Ilongero Wilaya ya Singida kuashiria uzinduzi rasmi wa shule hiyo ambayo ujenzi wake umegharimu kiasi cha zaidi ya Shilingi bilioni moja.


Shule hiyo mpya iliyojengwa ililenga kupunguza msongamano mkubwa wa wanafunzi katika shule ya sekondari Ilongero na kuwapunguzia adha wanafunzi kutembea umbali mrefu baadhi ya wanafunzi waliokua wakisoma shule ya Sekondari Ilongero imezinduliwa rasmi leo Oktoba 25, 2024.

Akizungumza maara baada ya kukagua majengo na kuweka jiwe la msingi katika shule hiyo Waziri Silaa amesema hiyo ni sehemu tu ya uwekezaji mkubwa unaofanywa na Serikali katika sekta ya elimu nchi nzima ikiwa ni pamoja na Mkoa wa singida.


Ametoa rai kwa wanafunzi wa shule hiyo mpya iliyoanza rasmi januari 2023 ikiwa na idadi ya wanafunzi 483 hadi sasa kuhakikisha wanasoma kwa bidii kwa kuwa tayari Serikali imeweka miundombinu bora katika shule hiyo.

Akitoa taarifa ya Mradi wa shule hiyo Mkuu wa Shule ya Sekondari Sekoutoure Tatu Njaku amesema ujenzi wa shule hiyo umeboresha mazingira ya Kufundishia na wanafunzi kujifunza.

Mkuu wa Mkoa wa Singida Halima Dendego kwa ujumla wake amesema kwa kipindi cha miaka Mitatu ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan, Mkoa wa Singida unashule mpya za sekondari 33 ikiwa ni kuendelea kupunguza changamoto za wanafunzi kusoma umbali mrefu. </

Post a Comment

0 Comments