Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi amewasili mkoani Tabora kwa ajili ya ziara ya siku mbili, ambapo baada ya kutua Uwanja wa Ndege wa Tabora, na kupokelewa na wenyeji wake, waliiongozwa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tabora Ndugu Said Juma Nkumba, Balozi Nchimbi alipata nafasi ya kupokea taarifa ya utendaji wa kazi wa Chama kutoka kwa Katibu wa CCM Mkoa wa Tabora, Ndugu Wilson Nkhambaku na taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya Mwaka 2020 - 2025, kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Mhe. Paulo Matiko Chacha, leo tarehe 19 Disemba 2024.
0 Comments