KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi akiwasili na kupokelewa Wilaya ya Nzega, leo Ijumaa tarehe 20 Desemba 2024. Kabla ya kushiriki Mkutano Mkuu wa Jimbo la Nzega mjini, ambao amealikwa kuwa mgeni rasmi, Balozi Nchimbi alifanya uzinduzi wa ukumbi mkubwa wa mikutano unaomilikiwa na CCM Wilaya ya Nzega, wenye uwezo wa kutumiwa na watu takriban 1,500 - 1,900 wakiwa wamekaa, ulioko Ofisi ya CCM Wilaya ya Nzega.
0 Comments