KAMPUNI ya Bima za Maisha ya Jubilee (Jubilee Life Insurance) imefanikiwa kushinda tena tuzo za Consumer Choice Awards Africa 2024 ikiwa ni 'Most Reliable Life Insurance Company in Tanzania'
Akizungumza na waandishi wa habari, Mkurugenzi Mtendaji wa Jubilee Life Bi. Helena Mzena wamewapongeza waandaji wa tuzo hizo kwa kuona kazi nzuri ambayo Kampuni hiyo inafanya ya kuwahudumia wateja na bima bora za Maisha.
Aidha ametoa shukurani za dhati kwa Wateja ambao ndiyo muhimili wa utenda kazi wao kwa kutenga muda wao na kuipigia kura Jubilee Life Insurance .
Pamoja na hayo wanaaipongeza Timu nzima ya Jubilee Life Insurance kwa jitihada na kujitoa kwao kwa hali na mali katika kuwahudumia wateja.
"Ahadi yetu ni kuendelea kutoa huduma bora, za uhakika na za kuaminika kwa wateja wetu ili kuendelea kulinda ndoto zao pamoja na wapendwa wao" amesema Bi. Mzena
0 Comments