Ticker

    Loading......

KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA YA MAMA SAMIA YAPATIWA MAGARI 10


Waziri wa Katiba na Sheria Dk. Damas Ndumbaro,akizindua magari 10 kwa ajili ya Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia (MSLAC) ili kuongeza kasi ya utoaji huduma hiyo kwa watanzania hafla iliyofanyika leo Disemba 20,2024 jjijini Dodoma.

Na Mwandishi Wetu, DODOMA

RAIS Samia Suluhu Hassan ametoa magari 10 kwa Wizara ya Katiba na Sheria kwa ajili ya Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia (MSLAC) ili kuongeza kasi ya utoaji huduma hiyo kwa watanzania.

Akizungumza leo Disemba 20,2024 jjijini Dodoma kwenye hafla ya kukabidhi magari hayo, Waziri wa Katiba na Sheria Dk. Damas Ndumbaro alimshukuru Rais Samia kwa namna anavyowawezesha kutekeleza program mbalimbali ikiwamo kampeni hiyo ambayo hadi sasa imefikia mikoa 11 ya Morogoro,Manyara,Singida,Mara,Simiyu.Ruvuma ,Shinyanga ,Iringa, Songwe,Dodoma na Njombe .

“Kwenye mikoa hii 11 tuliyofika tumebaini njaa na kiu ya haki kwa watanzania ni kubwa sana na sasa kupitia vitendea kazi hivi kampeni itafikia mikoa sita kwa wakati mmoja ili kukidhi kiu ya haki kwa watanzania,”alisema.

Aliongeza kuwa “Magari hayo dhumuni lake ni kusaidia watendaji wa Wizara pamoja na wadau wengine wanaoshirikiana nao kwenye kampeni hiyo ili kuwafikia watanzania katika kona zote za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kukidhi kiu yao ya kupata haki, elimu ya sheria na Katiba.”

Alitoa rai kwa madereva kutunza vizuri magari hayo ili kuwafikia watanzania wengi zaidi.

“Tuna kila sababu Katibu Mkuu na watendaji wako katika kampeni hii kufanya mikoa sita kwa wakati mmoja, tulikuwa awali hatuwezi kwasababu ya vitendea kazi, ili kukamilisha kuizunguka mikoa yote ifikapo Machi 2025,”alisema.

Alisema kwenye maeneo ambayo yamefikiwa na kampeni hiyo wameona kuna uhitaji wa kurudi tena hasa migogoro ya wakulima na wafugaji na vizuizini yaani kwenye magereza.

Awali, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Eliakim Maswi alisema magari hayo yamenunuliwa kwa fedha za serikali kwa ajili ya kazi maalumu.

Maswi alisema magari hayo yatasaidia pia watumishi wa Wizara hiyo kutekeleza majukumu yao ya kawaida na kutoa masaada wa kisheria.

“Mabasi haya mawili yatatumika kubeba watumishi kwenye shughuli za kampeni tunapokwenda mikoani kutoa uelewa na uwezesho wa masuala ya kisheria,”alisema.

Alisema magari hayo yanatumia mafuta kidogo hiyo yatapunguza gharama za uendeshaji.


Waziri wa Katiba na Sheria Dk. Damas Ndumbaro,akikata utepe kuashiria uzinduzi wa magari kwa ajili ya Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia (MSLAC) ili kuongeza kasi ya utoaji huduma hiyo kwa watanzania hafla iliyofanyika leo Disemba 20,2024 jjijini Dodoma.



Waziri wa Katiba na Sheria Dk. Damas Ndumbaro,akizindua magari 10 kwa ajili ya Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia (MSLAC) ili kuongeza kasi ya utoaji huduma hiyo kwa watanzania hafla iliyofanyika leo Disemba 20,2024 jjijini Dodoma.


Waziri wa Katiba na Sheria Dk. Damas Ndumbaro,akiwa ndani ya gari mara baada ya kuzindua magari 10 kwa ajili ya Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia (MSLAC) ili kuongeza kasi ya utoaji huduma hiyo kwa watanzania hafla iliyofanyika leo Disemba 20,2024 jjijini Dodoma.


MUONEKANO wa magari 10 yaliyokabidhiwa kwa Wizara ya Katiba na Sheria kwa ajili ya Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia (MSLAC) ili kuongeza kasi ya utoaji huduma hiyo kwa watanzania hafla iliyofanyika leo Disemba 20,2024 jjijini Dodoma.


Waziri wa Katiba na Sheria Dk. Damas Ndumbaro,akizungumza na waandishi wa habari wakati wa hafla ya kupokea magari 10 kwa ajili ya Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia (MSLAC) ili kuongeza kasi ya utoaji huduma hiyo kwa watanzania hafla iliyofanyika leo Disemba 20,2024 jjijini Dodoma.


Katibu Mkuu wa Wizara Wizara ya Katiba na Sheria Bw.Eliakim Maswi,akielezea jinsi magari hayo yatakayosaidia kutoa huduma kwa wananchi kwa haraka.

Post a Comment

0 Comments