Ticker

6/recent/ticker-posts

LALJI FOUNDATION YATOA MSAADA WA VIUNGO BANDIA HOSPITALI YA CCBRT

Jamii imeaswa kujenga utamaduni wa kutoa msaada kwa watu wenye mahitaji maalumu ikiwepo watu wenye mahitaji ya viungo bandia kutokana na gharama ya upatikanaji wa viungo hivyo na wenye uhitaji kushindwa kumudu gharama.

Wito huo umetolewa na Mkurugenzi mtendaji wa taasisi ya LALJI FOUNDATION Bi. Fatma Mussa wakati akikabidhi msaada wa viungo bandia kwa wagonjwa 11 katika Hospitali ya CCRBT Dar es salaam leo Jumatano Desemba 18,2024.

Akizungumza mara baada ya kukabidhi msaada huo amesema lengo ni kugusa watu wenye mahitaji mbalimbali katika jamii ambapo pia amewataka wadau na watanzania kwa ujumla kujitokeza kwa wingi ili kuunga mkono juhudi hizo.

Hii ni mara ya tatu kwa taasisi ya LALJI FOUNDATION kutoa msaada kwa wagonjwa wenye uhitaji wa viungo bandia hospitali ya CCBRT ikiwa ni utamaduni wa taasisi hiyo kusaidia watu wenye uhitaji.

Post a Comment

0 Comments