Ticker

6/recent/ticker-posts

MAHAFALI YA 22 TIA YAFANA, YAPONGEZWA KUENDELEZA UBUNIFU

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

TAASISI ya Uhasibu Tanzania (TIA) imepongezwa kwa kuwa mstari wa mbele kupitia mpango wa vituo atamizi, unaowawezesha wanafunzi kujiajiri, kuajirika, na kuchangia uchumi wa taifa.

Aidha, wamepongezwa kwa kuwaendeleza wanafunzi wenye mawazo ya kibunifu ili waweze kufanikisha malengo yao.

Pongezi hizo zimetolewa leo Desemba 13, 2024 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Jenifa Omolo akimwakilisha Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Nchemba kama mgeni rasmi katika Mahafali ya 22 ya Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) katika Kampasi ya Dar es Salaam.

Amesema katika ulimwengu wa sasa wa teknolojia, amewasihi wahitimu kutumia ubunifu wao kutatua changamoto na fursa za kijamii.

"Mitandao ya kijamii ni rasilimali yenye nguvu. Itumieni kwa njia chanya kama vile kujifunza, kujitangaza kibiashara, na kujipatia kipato". Amesema.

Amesema TIA ni miongoni mwa taasisi zilizowezeshwa jumla ya shilingi za Kitanzania Bilioni 58.1, kwa ajili ya kukamilisha miradi mbalimbali ya maendeleo hususan ujenzi wa miundombinu ya kusomea na kufundishia.

Aidha ameupongeza uongozi na watumishi wa TIA kwa kuhakikisha miradi hii inatekelezwa kwa wakati.

"Niwasisitize kuhakikisha inawekwa mipango Madhubuti ya kutunza miundombinu hiyo". Amesema

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Wizara Profesa Jehovaness Aikael ameipongeza Serikali kwa juhudi zake kubwa katika kuboresha mazingira ya kujifunzia na kufundishia kupitia ujenzi wa miundombinu katika Kampasi zake za Mbeya, Mtwara, Mwanza, Singida na Zanzibar.

Pamoja na hayo amewaasa wahitimu kuwa mabalozi wazuri wa TIA kwa kuonesha uadilifu na ufanisi. "Peperusheni bendera ya TIA kwa mafanikio, na endeleeni kuwa mfano wa kuigwa katika jamii na sehemu za kazi".


Naye Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) Prof. William Pallangyo, amesema kuwa kumekuwa na ongezeko la idadi ya Wanafunzi mwaka hadi mwaka hilo limechangiwa na kuongezeka idadi ya wanufaika wa mikopo kupitia Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB).


Hata hivyoamesema kuwa katika mwaka wa masomo 2024/2025, jumla ya wanachuo 12,263 wamenufaika na mkopo wenye thamani ya takribani shilingi bilioni 7.49 kiasi ambacho ni sawa na ongezeko la asilimia 35.9 ikilinganishwa na wanachuo 9,025 katika mwaka wa masomo 2023/2024, waliopokea jumla ya shilingi bilioni 6.14.

Ameeleza kuwa ni hatua muhimu inayotimiza dhamira ya TIA ya kufikisha huduma karibu na wananchi kupitia Kampasi zake zilizopo Kanda zote za Tanzania.


Amesema kuwa Kampasi hizo zenye jumla ya Wanachuo 31,084, zipo kimkakati katika Mikoa ya Dar es Salaam (Kanda ya Pwani), Singida (Kanda ya Kati), Mbeya (Kanda ya Nyanda za Juu usini), Mtwara (Kanda ya Kusini), Mwanza (Kanda ya Ziwa), Kigoma (anda ya Magharibi), Tanga (Kanda ya Kaskazini), na Zanzibar.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bi. Jenifa Christian Omolo, akimkabidhi cheti cha pongezi kwa kufanya vizuri katika masomo yake ya Rasilimali Watu, Bi. Naf-hat fahmi Hamed, wakati wa Mahafali ya 22 ya Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) katika Kampasi ya Dar es Salaam Viwanja vya Kurasini ambayo ni Makao Makuu ya Taasisi hiyo.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Bi. Jenifa Christian Omolo, akizungumza na hadhara wakati wa Mahafali ya 22 ya Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) katika Kampasi ya Dar es Salaam Viwanja vya Kurasini ambayo ni makao makuu ya Taasisi hiyo.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bi. Jenifa Christian Omolo, akiteta jambo na Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) Prof. William Pallangyo, wakati wa Mahafali ya 22 ya Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) katika Kampasi ya Dar es Salaam Viwanja vya Kurasini ambayo ni makao makuu ya Taasisi hiyo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Taasisi ya Uhasibu, Prof. Jehovaness Aikael, akizungumza na hadhara wakati wa Mahafali ya 22 ya Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) katika Kampasi ya Dar es Salaam Viwanja vya Kurasini ambayo ni Makao Makuu ya Taasisi hiyo.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Bi. Jenifa Christian Omolo (katikati), akiwa katika maandamano ya Mahafali ya 22 ya Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) katika Kampasi ya Dar es Salaam Viwanja vya Kurasini ambayo ni Makao Makuu ya Taasisi hiyo. Kushoto ni Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) Prof. William Pallangyo na kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Taasisi ya Uhasibu Prof. Jehovaness Aikael.
Baadhi ya wahitimu wakiwa wamesimama wakisubiri kutunukiwa shahada mbalimbali katika Mahafali ya 22 ya Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) katika Kampasi ya Dar es Salaam Viwanja vya Kurasini ambayo ni makao makuu ya Taasisi hiyo.

Post a Comment

0 Comments