Ticker

6/recent/ticker-posts

SERIKALI YASEMA UNYANYASAJI DHIDI YA WENYE ULEMAVU SASA BASI

-Dkt. Biteko asema Serikali itakula Sahani moja na wanyanyasaji wa wenye ulemavu

-Wakuu wa Mikoa waagizwa kusimamia mpango wa taifa haki na Ustawi kwa wenye ulemavu

- Halmashauri zatakiwa kutenga Bajenti ununuzi wa teknolojia saidizi kwa wenye ulemavu


Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amesema Serikali haipendi kusikia na haitavumilia kusikia uwepo wa vitendo vya unyanyasaji kwa watu wenye ulemavu na wale watakaojihusisha na vitendo hivyo itawachukulia hatua kikamilifu.

DKt. Biteko amesema hayo Jijini Dar es Salaam wakati akimwakilisha Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa katika maadhimisho ya Siku ya watu wenye ulemavu iliyofanyika sambamba na uzinduzi wa Mpango Kazi wa Taifa wa Haki na Ustawi wa Watu wenye Ualbino na Mkakati wa Taifa wa Teknolojia Saidizi kwa wenye ulemavu.

“Hatuwezi kuvumilia kuona watu wanaojihusisha na vitendo vya unyanyasaji wa watu wenye ulemavu, eti wananauza viungo vya albino, au wanafanya mauaji, nawahakikishia tutakula nao Sahani moja!,” amesema Dkt. Biteko.

Amesema Kauli mbiu ya mwaka huu: ‘Kukuza uongozi kwa watu wenye ulemavu kwa ajili ya mustakabali Jumuishi na endelevu ni muafaka kwa vile inaendana na tamko la kimataifa la kukuza ufahamu wa jamii kuhusu haki za watu wenye ulemavu duniani.

Dkt. Biteko ameongeza kuwa Serikali imeweka miongozo mbalimbali ikiwemo kutenga fedha kwa ajili ya makundi maalum ikiwemo watu wenye ulemavu.

“ Kitengo cha Ufuatiliaji na tathimini kiko ndani ya Ofisi hii ya Waziri Mkuu, kifanye ufuatiliaji kujua Ofisi na halmashauri zinavyotenga fedha kwa ajili ya makundi maalum na tupate taarifa ya ufuatiliaji wake,” amesisitiza Dkt. Biteko.

Amesema haipendezi kuona tunakubaliana na kuweka maazimio ya kazi lakini utekelezaji wake unabaki katika makablasha.

Aidha, amewaelekeza Wakuu wa wote wa Mikoa nchini kutekeleza mpango kazi wa haki na ustawi kwa watu wenye ualbino na kuhakikisha unatekelezwa kikamilifu, kuhakikisha kila halmashauri nchini inatenga bajeti ya ununuzi wa Vifaa saidizi kwa kuzingatia uhitaji na viwango vya ubora wa Vifaa hivyo na Wizara za kisetka kutekeleza Mpango na mkakati huo kwa mujibu uliowekwa na Ofisi ya Rais, TAMISEMI.

Kwa upande wake, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Watu wenye ulemavu, Mhe. Ridhiwan Kikwete, amesema Serikali inafanya jitihada za kuhakikisha jamii inatambua haki za kijamii kwa watu wenye ulemavu na ndiyo msingi wa kuzinduliwa kwa mkakati huo.

Naye Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge, Mhe. Riziki Lulida amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa jitihada za kuwawezesha nakuwakomboa watu wenye ulemavu kwa maendeleo endelevu na jumuishi.

“Katika kipindi cha miaka minne ya uongozi wa Rais Samia walemavu wanaunga mkutano jitihada za matumizi ya nishati safi pamoja na kushiriki katika shughuli mbalimbali ikiwemo uchimbaji wa madini katika migodi,” amesema na kuongeza kuwa wanazidi kumuunga mkono Rais ili atekeleze maono yake.

Mkurugenzi Mtendaji wa HelpAge Tanzania, Smart Daniel amesema kila binadamu anavyo vigezo vya kuwa mlemavu maishani kwa kuzaliwa, kupata ajali au kuzeeka na baadhi ya viongo kushindwa kufanya kazi kawaida.

Post a Comment

0 Comments