WAZIRI wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Selemani Saidi Jafo,leo Disemba 12,2024 ameshiriki kikao cha Mawaziri cha kisekta chenye lengo la kuimarisha masuala ya kiuchumi kilichofanyika Jijini Addis Ababa, Ethiopia.
Katika Mkutano huo masuala mbalimbali ya kisera yamejadiliwa ili kuimarisha uchumi kupitia Biashara, Madini ya mkakati, na Utalii.
Dkt.Jafo akiwa na Naibu Waziri wa Madini Dkt. Steven Kiruswa pamoja na wataalam wa Viwanda, Madini, na watalaam wa wizara ya Utalii katika mkutano wa Afrika wa masuala ya Biashara, Madini na utalii katika Jiji la Addis Ababa Ethiopia.
0 Comments