Na; Mwandishi Wetu - DODOMA
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Ridhiwani Kikwete amewasilisha Muswada wa Marekebisho ya Sheria za Kazi (Na. 13) wa Mwaka 2024 (The Labour Laws Amendments (No.13) Bill, 2024) mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii, jijini Dodoma, leo Januari 14, 2025.
Aidha, Mhe. Ridhiwani Kikwete amesema Ofisi ya Waziri Mkuu itaendelea kusimamia uwepo wa mazingira mazuri ya kazi na kuhakikisha kwamba viwango vya kazi vinazingatiwa ili wananchi wafanye kazi zenye staha.
0 Comments