Na Oscar Nkembo
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Dkt. Seif Shekalaghe ameipongeza Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali kwa kazi kubwa ya kutekeleza majukumu yake kwa maslahi ya taifa.
Dkt. Shekalaghe ameyasema hayo leo katika hafla ya uzinduzi wa Bodi ya tatu ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali akimuwakilisha Waziri wa Afya, Jenisha Mhagama, iliyofanyika katika ukumbi wa Mkemia ulipo Ofisi ndogo za Mamlaka jijini Dar es Salaaam.
“Dhamana mliopewa ni kubwa sana na kazi inayofanyika ni kubwa sana na ni kazi ambayo ina maslahi mapana ya nchi na wale ambao wanatafuta haki zao, ni dhamana kubwa naomba muichukue na kuisimamia na kumtanguliza mwenyezi Mungu pale ambapo mnatekeleza majukumu yenu” alisema Dkt. Shekalaghe.
Katika hatua nyingine Katibu Mkuu amesema Serikali ya awamu ya sita chini ya Dkt. Samia Suluhu Hassan imejidhatiti kuhakikisha Mamlaka inafanya kazi kwa ufanisi kwa kuendelea kununua mitambo ya kisasa hali iliyosaidia kuondoa ucheleweshwaji wa matokeo na kuharakisha upatikanaji wa haki
Kwa Upande wake Mwenyekiti wa Bodi, Christopher Kadio, amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kumuamini na kumteua kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali.
“Kipekee nimshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuniamini na tunaishukuru sana Serikali ya awamu ya sita kwa kuiwezesha Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali kuendelea kutimiza majukumu yake na sisi tumejipanga kuhakikisha tunatoa ushauri wa kisera unaoendana na malengo ya Kiserikali” alisema Kadio
Kadio ameahidi kuwa bodi hiyo itaimarisha utendaji wa Mamlaka na Kusimamia utekelezaji wa maelekezo yanayolenga kuboresha huduma kwa wananchi kwa kutumia ujuzi maarifa na weledi na kufanikisha lengo la utoaji wa huduma bora na kwa wakati kwa watanzania wote.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Dkt. Seif Shekalaghe, akitoa hotuba kwa niaba ya Waziri wa Afya, Mhe. Jenista Mhagama, katika hafla ya uzinduzi wa bodi ya tatu ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali iliyofanyika katika ukumbi wa Mkemia jijini Dar es salaam, Februari 19, 2025.
Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka, Christopher Kadio, akitoa neno la shukrani katika hafla ya uzinduzi wa bodi ya tatu ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali iliyofanyika katika ukumbi wa Mkemia jijini Dar es salaam, Februari 19, 2025.


Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko (aliyesimama) akieleza majukumu ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali katika hafla ya uzinduzi wa bodi ya tatu ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali iliyofanyika katika ukumbi wa Mkemia jijini Dar es salaam, Februari 19, 2025. Katikati ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Dkt. Seif Shekalaghe na kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi, Christopher Kadio

Baadhi ya Wajumbe wa Bodi ya tatu ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali, wakimsikiliza Mgeni rasmi (hayupo pichani) alipokuwa akiwasilisha hotuba yake katika hafla ya uzinduzi wa bodi ya tatu ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali iliyofanyika katika ukumbi wa Mkemia jijini Dar es salaam, Februari 19, 2025.

Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Dkt. Seif Shekalaghe (katikati) akikata utepe wa uzinduzi wa bodi ya tatu ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali iliyofanyika katika ukumbi wa Mkemia jijini Dar es salaam, Februari 19, 2025. Kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi, Christopher Kadio, kulia ni Mkemia Mkuu wa Serikali Dkt. Fidelice Mafumiko.
0 Comments