Ticker

6/recent/ticker-posts

NACTVET KUSHIRIKIANA NA VIWANDA KUTIMIZA MATAKWA YA SERA MPYA YA ELIMU


Na.Alex Sonna-DODOMA

KAIMU Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET), Dkt. Amani Makota,amesema kuwa Baraza hilo linakusudia kufanya kazi kubwa zaidi na viwanda kwa ajili ya kutekeleza kwa usahihi Sera mpya ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 2014 toleo la mwaka 2023.

Dkt.Makota ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye banda la NACTVET katika Maonesho ya uzinduzi wa Sera ya Elimu na Mafunzo kwa mwaka 2014, toleo la 2023 katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma

Aidha amesema kuwa kazi kubwa ya baraza hilo ni kuhakikisha inafanya ambayo ni kuhakikisha inakuwa na usimamizi thabiti katika vyuo .

Amesema kuwa kutokana na kuwepo kwa hiyo sera mpya NACT VET imeboresha kwa mifumo ya Amali na mafunzo hayo yataenda hadi kwa ngazi ya sekondari.

"Sisi katika sera mpya kuna mambo muhimu ya kutekeleza ikiwa ni pamoja na kutimiza usimamizi licha ya kuwa usimamizi kwetu ni wa siku zote,lakini kwa sasa tumeboresha kwa mifumo.

"Sera mpya kwa sasa imesema mafunzo ya Amali yataenda hadi kwa ngazi ya sekondari,lakini kikubwa zaidi ni mageuzi ya kimitaala yanayokuja sasa,hivi kama baraza tunasisitiza sana upande wa Amali vijana watakuwa wanajifunza kuanzia ngazi ya sekondari wanapata ujuzi.

"Lakini kwa hivisasa kuna ushirikiano mkubwa na viwanda vyetu na mageuzi ambayo tumeyafanya sasa hivi tunataka hata kijana aliyotoka chuo kikuu akiona kuna ujuzi fulani kaukosa na anahuitaji aje katika vyuo vyetu vya Amali apate mafunzo ya Muda mfupi na baadaye akishapata mafunzo hayo basi akayatumikie"ameeleza Dkt.Makota

Hata hivyo ameeleza kuwa ukiangalia sera mpya ambayo imewafikia watanzania inaenda kubadilisha Uchumi na kukua kwa kasi zaidi huku akiendelea kusisitiza kuwa baraza linahitaji kufanya kazi na viwanda zaidi na kwa kasi kubwa ili kuonesha mabadiliko makubwa yanayotokana na sera hiyo.

Post a Comment

0 Comments